Elections 2010 Wabunge wa darasa la saba wataweza kuchangia hoja za kitaalam???

Common guys! Elimu na uongozi haziendani! Angalieni wasomi wetu wasivyokuwa na uadilifu.

Mrema Lyatonga alikuwa waziri wa mambo ya ndani na kila mtu aliona mchango wake! Alikuwa na degree ngapi hebu waacheni wafanye mambo wapimeni baada ya miaka 5.

John Major hakuwa na elimu kabisa, lakini alikuwa kiongozi wa conservative 1990-7 na waziri mkuu wa UK. Maprof wetu na maPhD wameifanyia nini Tanzania......Chenge?
 
Nimeona kwenye list ya wagombea wa CCM kuna wagombea kadhaa ambao elimu yao ni shule ya msingi, swali langu je hawa wakiwa kwenye kamati za bunge wataweza kutusaidia? Mfano mikataba karibu yote imeandikwa kwa kiingereza, na majarida mengi ya kitaalam pia yapo kwa kimombo je hawa watatoa michango gani kama hawataweza kuelewa kilichoandikwa??
  1. Jah People - Njombe Kaskazini
  2. Jamal Tamimu - Muhambwe
  3. Lameck Airo - Rorya
  4. Luckson Mwajale - Mbeya Vijijini
  5. Hussein Amar - Nyang'wale
  6. ........
  7. ........
Hivi kinachowafanya waharibu ni SHULE ZAO ........... au ............. TAMAA ZAO.........???
 
Kila kitu kina nafasi yake ktk maisha... tusiwadharau wasiokuwa na elimu ya juu kwani matajiri wakubwa duniani ni watu wasiokuwa na ELIMU kubwa...Kwa sababu hawa ni watu wanaochukua risk kubwa pasipo kupiga mahesabu makubwa ya kugawa na kutoa. Ni rahisi sana kumshawishi mtu asieenda shule kwa mambo muhimu ktk maisha kuliko msomi ambaye huwa na mlolongo wa list ya maswali mengi na mazito hata ikiwa ni kuchota maji mtungini na kunywa..

Kuna ushahidi mkubwa kwamba hata uongozi wa chama Republican cha Marekani kuna watu wabunge kibao ambao shule ilipita pembeni na wapo na wapo kiisha ndio wapambanaji wabaya kuliko wale wasomi ambao kwao hutumia zaidi sayansi hata mahala pa logic. Umuhimu ni kwamba mbunge anawakilisha wananchi wetu. Ikiwa asilimia 90 ya watu unaowawakilisha hawana elimu, hiyo Elimu yako haiwezi kuwasaidi ikiwa hufahamu mahitaji yao, sana sana utawazingua ni hicho kidhungu..
Yameanza kujitokeza huko Nzega..
 
kwakuwa hawa wasomi tuliowapeleka huko miaka yote hii hawajatusaidia bora tujaribu hawa std 7,
 
Nimeona kwenye list ya wagombea wa CCM kuna wagombea kadhaa ambao elimu yao ni shule ya msingi, swali langu je hawa wakiwa kwenye kamati za bunge wataweza kutusaidia? Mfano mikataba karibu yote imeandikwa kwa kiingereza, na majarida mengi ya kitaalam pia yapo kwa kimombo je hawa watatoa michango gani kama hawataweza kuelewa kilichoandikwa??
  1. Jah People - Njombe Kaskazini
  2. Jamal Tamimu - Muhambwe
  3. Lameck Airo - Rorya
  4. Luckson Mwajale - Mbeya Vijijini
  5. Hussein Amar - Nyang'wale
  6. ........
  7. ........

uzuri wa bunge letu halina tofauti na vikao vya harusi na kicheni pati,
hivyo nahisi hawatakuwa na taabu saaanaa, watakabiriana nalo tu,
mbona wabunge wasomi na ambao ndiyo wengine wanakuwa wasomi
ndiyo wanaongoza kwa kusaini mikataba mibovu, na kulizamisha taifa?

kikubwa ni kutowachagua wao sisiemu yao
 
Hapo umenena kweli
 
Afadhari sasa tunaenda kupima upande wa pili wa shilingi ...tulikuwa na maprof na madaktari hata wale wa kuchakachua elimu sasa tumepata 'maprofesa' wa mambo ya jadi /asilia wakisaidiana na wajasiliamali/wafanyabiashara wenye LY katika kusukuma gurudumu la uchumi wetu kupandisha kilima kikali cha muanguko wa shilingi. Labda watakuwa kisiwa[oasis] kwenye jangwa la mafisadi.
 
Kila kitu kina nafasi yake ktk maisha... tusiwadharau wasiokuwa na elimu ya juu kwani matajiri wakubwa duniani ni watu wasiokuwa na ELIMU kubwa...Kwa sababu hawa ni watu wanaochukua risk kubwa pasipo kupiga mahesabu makubwa ya kugawa na kutoa. Ni rahisi sana kumshawishi mtu asieenda shule kwa mambo muhimu ktk maisha kuliko msomi ambaye huwa na mlolongo wa list ya maswali mengi na mazito hata ikiwa ni kuchota maji mtungini na kunywa..

Kuna ushahidi mkubwa kwamba hata uongozi wa chama Republican cha Marekani kuna watu wabunge kibao ambao shule ilipita pembeni na wapo na wapo kiisha ndio wapambanaji wabaya kuliko wale wasomi ambao kwao hutumia zaidi sayansi hata mahala pa logic. Umuhimu ni kwamba mbunge anawakilisha wananchi wetu. Ikiwa asilimia 90 ya watu unaowawakilisha hawana elimu, hiyo Elimu yako haiwezi kuwasaidi ikiwa hufahamu mahitaji yao, sana sana utawazingua ni hicho kidhungu..
Yameanza kujitokeza huko Nzega..
hapo umenena kweli tupu mkuu
 
Nimeona kwenye list ya wagombea wa CCM kuna wagombea kadhaa ambao elimu yao ni shule ya msingi, swali langu je hawa wakiwa kwenye kamati za bunge wataweza kutusaidia? Mfano mikataba karibu yote imeandikwa kwa kiingereza, na majarida mengi ya kitaalam pia yapo kwa kimombo je hawa watatoa michango gani kama hawataweza kuelewa kilichoandikwa??
  1. Jah People - Njombe Kaskazini
    [*]Jamal Tamimu - Muhambwe
  2. Lameck Airo - Rorya
  3. Luckson Mwajale - Mbeya Vijijini
  4. Hussein Amar - Nyang'wale
  5. ........
  6. ........

Huyu niliyebold jina lake aliongoza kura za maoni za uhusikaji na viungo vya albino na bado kamati ya maadili CCM imemwona safi: PESA jamani zitatumalizia nchi yetu!!!
 
Kujifunza Kiingereza ukubwani si sawa na kuwa na elimu inayokuwezesha kufanya uchambuzi (analysis) wa maana kwenye miswada ya sheria.

Wapo waliodiriki hata kudanganya kwenye viapo vyao, wakadai kwamba wao wana elimu ya Sekondari (Form IV), kumbe ni Darasa la Saba!

Wamepitishwa kwa kuwa CCM haitaki wabunge wasomi, watakaoweza kuichambua miswada ya sheria ipasavyo, na kutoa hoja za maana zitakazoipa CCM wakati mgumu. Wanataka bunge litakalokuwa "rubber stamp", hawataki bunge lenye wapinzani - hata walio ndani ya CCM!

Watanzania mna kazi kubwa mwaka huu, kuliko miaka yote ya awali.

-> Mwana wa Haki

P.S. Wametoa rushwa ili wachaguliwe, fainali ni kwenda kusinzia bungeni na kula posho za bure! Wengi watakuwa na kesi za kutoa rushwa baada ya uchaguzi, wengi watashindwa, ushahidi unachukuliwa, unahifadhiwa, utatolewa mahakamani!
 
Back
Top Bottom