Wabunge wa Kigoma wana Matatizo gani?!

Maendeleo huletwa na watu na kazi ya serikali ni kuwawekea mazingira bora wananchi ili wajiletee maendeleo. Mazingira bora siyo kuwapa fedha, bali ni kuwapa Elimu na miundo mbinu.

Hapa kuna tunaozungumza tu kama kasuku, kuwa tatizo la mahali fulani ni la watu wenyewe kwa sababu wapenzi wetu wameguswa. Uchumi haujengwi na rasilmali peke yake, uchumi wa kisasa huhitaji miundo mbinu ili kuvutia mitaji itakayogeuza rasilmali hizo kuwa mali halisi. Kwenye eneo la miundo mbinu Kigoma nadhani ni ya mwisho. Hivi ni mkoa gani ambao wananchi wake walichangia kupeleka grid ya umeme? Ni mikoa gani ambayo wananchi wake walichangia kujengwa barabara?

Tukubaliane kuna tatizo na si la Kigoma pekee, ila tukubaliane matatizo yanazidiana na kwa kigoma ni mengi zaidi. Kwa hiyo mazingira yanazuia maendeleo hata hicho unachokiona ni kwa sababu wananchi ni very hardworking, achana na historia zilizozikwa makaburini za wanywa kahawa wa ujiji (ambao ni % ndogo mno).

Sasa suala la wabunge! Nikiri kuwa kwa kweli kwa wanaompenda Zitto wangemshauri vizuri zaidi. Sasa hivi uchaguzi unakaribia na lile si jimbo la kawaida. Fuatilia voting ya kigoma kaskazini au kigoma yote. Hawa wabunge watatu wa sasa (toa wale wa kasulu na kibondo), wana less than 10% ya kurudi Bungeni. Mnaompenda Zitto tafuteni hoja ya kumpa akauze Kigoma kaskazini, elfu mbili na kumi halioni bunge tena asilani.

Najua tutazuka na malalamiko cheap kuwa mafisadi wamemng'oa. Ukweli ni kuwa amepoteza mvuto jimboni kwake. Alipigiwa kura na wavuvi, ambao usalama ziwani ni kitu cha muhimu kuliko vyote, hawajamsikia akizungumzia mambo hayo, hata kama anazungumzia si vile wanavyotarajia. Alipigiwa kura na wakulima wa kahawa tarafa ya Kalinzi, hajawasaidi kurahisisha upatikanaji wa masoko, bila utapeli. Inawezekana anaungwa mkono na kina Alhaji Mahwisa, lakini power base ya Mahwisa imeshasambaratika. Zitto alipigiwa kura na wakulima wa michikichi wa tarafa ya Bitale, biashara zao zinadorora kwa sababu barabara hazipitiki. Hata huo UMEME SIYO AJENDA JIMBONI KWAKE. UMEME NI AJENDA JIMBONI KWA SERUKAMBA.

Napenda Zitto arudi Bungeni. Ndio maana natoa ushauri wa Bure. Suala hili la barabara ya manyovu CCM wameamua kudelay ili wammalize. Ninavyojua vile vile watavuruga kwenye malipo ya Fidia. Hilo litakuwa kaburi la mwisho la Zitto. Kama anataka urais, sawa, pengine ameshajijenga vya kutosha kitaifa. Lakini Jimboni kwake, his power base is eroded. ATAFUTE HOJA YA KUJIJENGA UPYA, VINGINEVYO ANAINGIA KWENYE SHIMO. ZITTO BILA UBUNGE IS NOTHING NA LAZIMA TUHAKIKISHE ANARUDI. VINGINEVYO AWAANGALIE KINA MBATIA.
 

Haswa wewe umenena vyema ila tu ni kwamba, FIDIA imeshavurugwa tayari ndugu yangu.

Wakati Zito anahangaikia 10% yake ya DOWNS wapiga kura wake wanalia kwani wameitwa kuchukua Cheque Bank bila hata uthamini kufanyika.

Habari ndio hiyo.
 

...inasikitisha sana, hata hivyo Mh. Zitto, mmoja wa wabunge machachari Tanzania alisema hatogombea tena ubunge 2010.

 

...mbona wana Kigoma tupo wengi tu humu,...

I hope wapinzani nao wanajipanga vizuri kutetea kiti cha ubunge wa Kigoma kaskazini 2010 mh.Zitto asiposimama...
 

Usiwe kwenye tuta Kigoma ni moja kati ya Mikoa yenye msimamo mkali wa utawala huu uliokuwepo ,hawautaki hata kuuona na ndio maana ukaona umetupwa kama kule Pemba Nchini Zanzibar ambayo imeungana na Tanganyika kuunda Jamhuri ya Shirikisho la Tanzania ,Kigoma waliwahi kkutishia ikiwa hawakupelekewa maendeleo basi watajitangaza kutaka kujitenga kama ilivyojitangaza Pemba ,kama nisemavyo kuwa popote pale ambapo pataonekana kuna upinzani wa uhakika basi serikali hii ya CCM haijishughulishi kupeleka maendeleo ya aina yeyote ile ,fanya upelelezi katika mikoa hiyo ukiwemo Tanga na Moshi pamoja na Nchi ya Zanzibar.

Kigoma ni moja ya sehemu ambayo CCM ilipoteza wabunge wengi katika uchaguzi Mkuu wa 2005 ,CCM hawajaweza tena kuirudisha Kigoma katika uchaguzi wa kihalali ni sawa na Nchini Zanzibar ambapo CCM haijaweza kujirudisha kupitia uchaguzi halali ,siku zote wanakimbia na masanduku ya kura.

Hivyo usiotegemee akina Zitto ambao tunawaona namna wanavyobadilika baada ya kutupiwa mfupa na hivyo kutopelekea kutetea kilichomfanya achaguliwe ,ila kesho kutwa atarudi tena huko kuja kuwaomba kura tena ,sijui mtamuuliza masuala gani ya kimaendeleo kuhusiana na mkoa wake ambayo ataweza kuyajibu na kuwafanya mumrudishe tena kweny jukwaa la ubunge.
 
Je ni kweli Zitto amesha tangaza kuwa hato gombea tena Ubunge.?
Niliwahi kusikia tetesi kama hizo
 

Nasikia harufu ya kaufisadi vile au? Ni mapambano kati ya haki na ufisadi. Haya ndiyo matokeo..............!!!!?????? Pole mafisadi mmekwisha!
 
Naomba kuwajulisha kuwa tatizo la wabunge wa Kigoma si la kuangalia kijuu juu tu. Sisi ambao ni wananchi wa Kigoma tunaoishi Kigoma tunajua kuwa tatizo la wabunge wetu ni zito kidogo.

Tatizo la kwanza ambalo pia ni la kimsingi hapa ni kuwa wabunge wa Kigoma wameendelea kurithi zile tabia za sisi watu wa Kigoma za kutoshirikiana, japo hawa ni watu waliokuwa wanapiga kampeni nzito nzito za kusaidia maendeleo ya Kigoma.

Pamoja na wabunge waliotajwa hapo wapo vile vile Mh. Nsanzugwanko wa Kasulu ambaye kila anapokuja katika jimbo lake la Kasulu anakuja kutengeneza maadui zake kwa lugha za kashifa na matusi. Hana lolote analolifanya; hatujawahi kusikia hata siku moja kwamba na mbunge huyu amewahi kuchangia kwa kuhamasisha shuhuli za maendeleo katika jimbo lake kama wanavyofanya wabunge wengine nchini. Mh. Mporogomyi, hali kadhalika, Mh. Kijiko na hao wenzake wako vile vile.

Mimi sishangai kwa kuwa hata watu wa Kigoma wenye uwezo wameuacha mkoa wao na watu wake wajihangaikie. Watu wa Kigoma wanapiga kura zao kutimiza haki yao kikatiba; huku wakijua kuwa wanawapatia KULA hao waheshimiwa, ila hakuna watakachokiona katika utawala wao. This is what prevails in so many minds of lots of people of Kigoma.

Serukamba ninamfahamu tangu shuleni, hawezi kubadilika; yeye ni wa hivyo hivyo.

Ninampongeza Zito kwa kuwa anajitahidi kwa kazi anayofanya, labda sasa atawageukia wapiga kura wake baada ya ku -fight kwa nchi nzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…