KipimaPembe
JF-Expert Member
- Aug 5, 2007
- 1,285
- 698
Maendeleo huletwa na watu na kazi ya serikali ni kuwawekea mazingira bora wananchi ili wajiletee maendeleo. Mazingira bora siyo kuwapa fedha, bali ni kuwapa Elimu na miundo mbinu.
Hapa kuna tunaozungumza tu kama kasuku, kuwa tatizo la mahali fulani ni la watu wenyewe kwa sababu wapenzi wetu wameguswa. Uchumi haujengwi na rasilmali peke yake, uchumi wa kisasa huhitaji miundo mbinu ili kuvutia mitaji itakayogeuza rasilmali hizo kuwa mali halisi. Kwenye eneo la miundo mbinu Kigoma nadhani ni ya mwisho. Hivi ni mkoa gani ambao wananchi wake walichangia kupeleka grid ya umeme? Ni mikoa gani ambayo wananchi wake walichangia kujengwa barabara?
Tukubaliane kuna tatizo na si la Kigoma pekee, ila tukubaliane matatizo yanazidiana na kwa kigoma ni mengi zaidi. Kwa hiyo mazingira yanazuia maendeleo hata hicho unachokiona ni kwa sababu wananchi ni very hardworking, achana na historia zilizozikwa makaburini za wanywa kahawa wa ujiji (ambao ni % ndogo mno).
Sasa suala la wabunge! Nikiri kuwa kwa kweli kwa wanaompenda Zitto wangemshauri vizuri zaidi. Sasa hivi uchaguzi unakaribia na lile si jimbo la kawaida. Fuatilia voting ya kigoma kaskazini au kigoma yote. Hawa wabunge watatu wa sasa (toa wale wa kasulu na kibondo), wana less than 10% ya kurudi Bungeni. Mnaompenda Zitto tafuteni hoja ya kumpa akauze Kigoma kaskazini, elfu mbili na kumi halioni bunge tena asilani.
Najua tutazuka na malalamiko cheap kuwa mafisadi wamemng'oa. Ukweli ni kuwa amepoteza mvuto jimboni kwake. Alipigiwa kura na wavuvi, ambao usalama ziwani ni kitu cha muhimu kuliko vyote, hawajamsikia akizungumzia mambo hayo, hata kama anazungumzia si vile wanavyotarajia. Alipigiwa kura na wakulima wa kahawa tarafa ya Kalinzi, hajawasaidi kurahisisha upatikanaji wa masoko, bila utapeli. Inawezekana anaungwa mkono na kina Alhaji Mahwisa, lakini power base ya Mahwisa imeshasambaratika. Zitto alipigiwa kura na wakulima wa michikichi wa tarafa ya Bitale, biashara zao zinadorora kwa sababu barabara hazipitiki. Hata huo UMEME SIYO AJENDA JIMBONI KWAKE. UMEME NI AJENDA JIMBONI KWA SERUKAMBA.
Napenda Zitto arudi Bungeni. Ndio maana natoa ushauri wa Bure. Suala hili la barabara ya manyovu CCM wameamua kudelay ili wammalize. Ninavyojua vile vile watavuruga kwenye malipo ya Fidia. Hilo litakuwa kaburi la mwisho la Zitto. Kama anataka urais, sawa, pengine ameshajijenga vya kutosha kitaifa. Lakini Jimboni kwake, his power base is eroded. ATAFUTE HOJA YA KUJIJENGA UPYA, VINGINEVYO ANAINGIA KWENYE SHIMO. ZITTO BILA UBUNGE IS NOTHING NA LAZIMA TUHAKIKISHE ANARUDI. VINGINEVYO AWAANGALIE KINA MBATIA.