MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Sisi tulio na wake wa kabila tofauti na la kutoka nchi ingine tuna changamoto sio haba na hayo matamshi za chuki za baadhi ya "viongozi". Kila siku hapa kwangu linapita ni kama karne. Lakini lile umoja nimeunda ndani ya boma ni kila kitu. Wakileta ujinga yao kwangu, uwe nani, aisee, watayaona! Amani na umoja wa taifa huanzia kwako nyumbani. Ukieneza chuki na ukabila kwako, itaonekana kwa watoto wako, na matamshi yako. Amen.
Bora wewe una mke wa kutokea nje ya nchi nyingine, mimi hapa kabila langu Mkikuyu, mke wangu nusu Mjaluo nusu Mluhya, hivyo mkikinukisha kwa misingi ya kikabila siwezi kumtorosha kwenda aishi kwa Wakikuyu, hali kadhalika siwezi kutorosha watoto wangu waishi kwa kina mke maana wana damu ya Ukikuyu.
Hivyo inabidi kuishi maeneo yenye mchanganyiko wa makabila, japo mimi nimewekeza kidogo nje ya nchi, huwa nawahurumia watu wenye ndoa mchanganyiko kama yangu lakini wanaishi kitaani kabisa ambao hawana pa kukimbilia. Naomba tuhubiri amani, tukemee chuki za kikabila. Juzi nimemkemea jamaa yangu fulani aliponiletea hizo pumba za misifa ya kikabila.