Wabunge wa upinzani wavuruga kikao Albania

Wabunge wa upinzani wavuruga kikao Albania

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wabunge wa kambi ya upinzani nchini Albania wamevuruga kikao cha Bunge kupinga hatua ya kufungwa Gerezani Mbunge mwenzao kwa tuhuma za kusema uwongo.

Wabunge hao wamesema kufungwa kwa Ervin Salianji ni hatua iliyochochewa kisiasa na wameitisha maandamano makubwa ya kuufunga Mji Mkuu, Tirana, kuanzia wiki ijayo.

Kwa miaka kadhaa sasa, Chama cha upinzani cha kihafidhina cha Democratic nchini Albania kimekuwa kikitoa tuhuma Kwamba Chama Tawala cha Kisoshalisti kimechukua kwa nguvu madaraka yote, yakiwemo ya Mahakama.

Chama hicho cha upinzani kimekuwa kikiendesha maandamano ya vurugu ya kuipinga Serikali tangu Mwaka 2013.


Katika tukio la Jumatatu (Septemba 30), Wabunge wa Chama hicho walimshambulia Spika pamoja na Mawaziri wa Serikali kwa Kuwarushia vitu pamoja na kuchoma moto viti.

Video: AP
 
Back
Top Bottom