Wabunge wa UVCCM Wachangia Milioni 30 Kwaajili ya Ujenzi Chuo cha UVCCM Tunguu, Zanzibar

Wabunge wa UVCCM Wachangia Milioni 30 Kwaajili ya Ujenzi Chuo cha UVCCM Tunguu, Zanzibar

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotokana na Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar, walifika katika chuo Cha Umoja wa Vijana Tunguu Kwaajili ya Uvunaji wa mabilinganyi na pilipili Boga Kwa lengo la kuendeleza Siasa na Uchumi Katika Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM.
WhatsApp Image 2024-12-31 at 08.59.01.jpeg

Aidha, Wabunge na wakilishi hao walipata nafasi ya kuzungumza ambapo; Mhe. Hudhaima Mbarak alisema, "Kwa kweli tumejionea kazi kubwa inayofanywa na Viongozi wetu mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Kwa kweli Maendeleo yao tunayaona katika Kila sekta"
WhatsApp Image 2024-12-31 at 08.59.02.jpeg

"Sisi wabunge na wakilishi tumeamua Kwa dhati kabisa kuwaunga Mkono Viongozi wetu haya Kwa Kuchangia Ujenzi huu Unaoendelea apa katika chuo chetu Cha Umoja wa Vijana, Kwa kutoa Shilingi Milioni 30 ili Sasa vijana wenzetu wajifunze hapa Itikadi ya historia ya Chama chao pendwa Cha CCM".
WhatsApp Image 2024-12-31 at 08.59.02 (1).jpeg
WhatsApp Image 2024-12-31 at 08.59.01 (1).jpeg

Imetolewa na Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi, Afisi kuu UVCCM Zanzibar .
 
Back
Top Bottom