Wabunge wa viti maalum kaeni kimya kuficha udhaifu wenu

Wabunge wa viti maalum kaeni kimya kuficha udhaifu wenu

Viti maalumu ni vya kina mama kujaribu ku-balance mfumo dume, na unajua hulka ya kina mama ni kudemka.....basi waache wademke kwani nini bhana...
Unataka kusemaje kuhusu Ile viti maalum ya Bashiru na Polepole mkuu?😃😃
 
Hivi viti maalumu vinasaidia nini? Vinajaza watu wengi bungeni bila sababu
 
Siyo majambazi, mafisadi na wachezea mifumo ya serikali tu wanaomjaribu rais Samia hata Chadema wanamjaribu.

Leo wametangaza maandamano ya kudai katiba mpya na tume huru yani wanataka rais aache kufocus na kukamilisha SGR ,Bwawa la nyerere ,ajira, viwanda ambavyo ndiyo hitaji la wananchi akaanze kutenga mabilioni ya fedha kwa ajili ya katiba ambayo ni hitaji la wanasiasa tu?

Mbaya zaidi wanataka mchakato wa katiba uanze upyaaaaa na siyo pale ulipoishia zamani
Madaraja, mabwawa, sgr zihitaji Katiba mpya
 
Kinuju, tofauti yako na zero brain ni haipo.
 
Kama mtoa mada unalenga hoja ya Mwanaisha Ulenge, utakuwa umefeli kwani alichokisema ni kweli, chombo cha kuisimamia serikali kinafanya kazi yake sawasawa?
 
Viti maalum vifutwe, ni matumizi mabaya sana ya pesa za walipa kodi.
Ni matumizi mabaya ya nguvu kazi, watu wanalipwa pesa nyingi kwa kupiga meza. Nguvu hiyo ingetumika shambani ingefaa.
 
Tangu wiki hii ianze tumeshuhudia ushauri wa ajabu sana kutoka kwa Wabunge wa viti maalum. Kila wanachoongea ni pumba tupu hadi unajiuliza hawa watu walipatikana vipi.

Ushauri wangu kaeni kimya maadam mshahara wa milioni 11 unaingia kila mwezi. Biblia imeandika "HATA MPUMBAVU AKINYAMAZA HUHESABIWA HEKIMA".

Fuateni nyayo za baadhi ya wabunge wenzenu humo, hawajawahi kuchangia chochote kwao bora kugonga meza kuliko kusimama na kuongea " utumbo wa kuku".
Hivi viti vifutwe wagombee majimboni
 
Back
Top Bottom