Tetesi: Wabunge wa viti maalumu wa CCM kutakiwa kugombea majimboni, bunge lijalo viti hivyo ni kwa wanawake wasomi wenye maono

Tetesi: Wabunge wa viti maalumu wa CCM kutakiwa kugombea majimboni, bunge lijalo viti hivyo ni kwa wanawake wasomi wenye maono

Ndio taarifa zinazosikika jijini Dodoma kwamba wabunge wote wa viti maalumu na wale wa kuteuliwa sasa wameshapata uzoefu wa kibunge hivyo chama kitawataka wakatafute majimbo wagombee.

Bunge lijalo linategemewa kuwa na wabunge wa viti maalumu wote wapya waliosheheni sifa za kisomi na ubobezi mbalimbali.

Taarifa zinadai kuna wakati Rais Magufuli anapata wakati mgumu kupata wateule sahihi wa nafasi za uwaziri kwa kuwa wale waliopo wanakuwa wamepungukiwa sifa za kiuteuzi.

Ni hayo kwa uchache.

Endelea kunywa mtori nyama utazikuta chini.

Maendeleo hayana vyama!
hii imekaa vizuri!
 
Yohana mbatizaji. Hata hivyo viti maalumu vilitakiwa vigombewe kati ya wanawake wa vyama tofauti, badala ya kuwa hisani ya viongozi wa vyama kwa kina mama eg Kenya
 
Sijasoma, but I have got vision....wanajamii mtanichagua ????!!!!!! 🙄🙄☺️☺️🙈🙈🙈
 
Badala ya chadema kuwajadili ccm ilitakiwa iwapongeze na kuiga mfano wao kwani wana wabunge wa viti maalumu wana zaidi ya mihula mitatu wala hawana mawazo ya kugombea
 
Kwakifupi basi limeshajaa. Wengi wataachwa kwenye vituo. Dereva ana majina ya Abiria Wake wote mkononi. Ni suala la muda tu.
 
Kwangu wa jimbo kapitishwa wa ameishia darasa la nne hata kiswahili kuongea shida
 
Back
Top Bottom