Wabunge wa Yanga walipa Goli 5 za Simba

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Wabunge wa Yanga wamewafunga wabunge wa Simba kwa idadi ya magoli 5 na kuwasaidia Young African club kulipa goli 5 walizofungwa na Simba tarehe 6 Mei 2012.

Nlichokiona kwa mpira walionyesha wabunge inaonesha Tanzania ya Zamani ilikua na wacheza wazuri sana kuanzia miili ya kimichezo mpaka uzalendo.

Kuna beki moja ya wabunge wa Yanga ndo alikua captain anasifa zote za kuwa beki yaonesha zama zake washambuliaji walipata shida sana kumpita au hata kumsogolea walikua hawamsogelei..

Wachezaji wa leo wajifunze kutoka kwa wakongwe hawa tena mpira wa sasa pesa zipo za kutosha.

Je kushinda leo kwa wabunge imetupa mwanga/taswira ya kitakachotokea 1 octoba 2016???..
 
Taswira ya kiuhalisia ni Yanga kapigwa cha nguruwe na Stand utd, na MNYAMA jana kaua kuelekea jumamosi, hiyo ndo taswira!!
 
Yanga kwa kujifariji..yani kufungwa leo mmechanganyikiwa mpaka wengine wanasema wachezaji wa Azam watimuliwe kisa wamefungwa na Ndanda sasa hayo matope au akili
 
Ayaone sembo leo siku imeenda vema..Mashabiki wa Yanga leo wanakuja na stori nyingi
Kwenye mpira kuna matokeo matatu...kushinda,kushindwa au kwenda sare matokeo ya leo tumeyapokea kama changamoto tukutane moja octoba.
 
Yanga kwa kujifariji..yani kufungwa leo mmechanganyikiwa mpaka wengine wanasema wachezaji wa Azam watimuliwe kisa wamefungwa na Ndanda sasa hayo matope au akili
Sidhani kama kuna shabiki wa Yanga ataandika mambo ya Azam humu...
 
Taswira ya kiuhalisia ni Yanga kapigwa cha nguruwe na Stand utd, na MNYAMA jana kaua kuelekea jumamosi, hiyo ndo taswira!!
Yote ni matokeo ndugu,Simba ametoka kweli kwenda viwanja vya mikoani?nakumbuka mwaka jana Yanga alicheza game 6 taifa simba wakaongea sana ila leo Yanga anafanya yake
 
Kuna mwenzio kaanzisha uzi kachanganyikiwa na kufungwa goli moja
Yote ni matokeo hakuna haja ya kupanic kwan hata stand wamecheza ili kushinda na ligi bado ndefu jst wait and see mwenye kisu kikali ndo atakula nyama
 
Yote ni matokeo hakuna haja ya kupanic kwan hata stand wamecheza ili kushinda na ligi bado ndefu jst wait and see mwenye kisu kikali ndo atakula nyama
Sawa wazee wa kimataifa hewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…