Wabunge waelewe Wakenya ndiyo wawekezaji wakubwa Tanzania

Wabunge waelewe Wakenya ndiyo wawekezaji wakubwa Tanzania

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,780
Reaction score
15,488
Wakati Watanzania sio wawekezaji wakubwa Kenya . Wakenya ndiyo wawekezaji wakubwa Tanzania na wanunuzi wakubwa na nafaka zetu za kilimo. Cha ajabu wabunge badala ya kuweka nchi mbele wanajiingiza kwenye kiki na uchawa ambao hauna msingi.

Wamesahau kabisa ni sawa na kuanza kumtukana mteja wako mwenyewe!. Hawa wakenya na Waganda wanaharakati walikuwa kwenye kesi wangeingia na kuondoka kama watu wengine waangalizi.

Badala yake Serikali imewapandisha zaidi ya ulazima na kuweka tafuruki zisizo na manufaa yeyote kwa taifa leo.

Huwezi tu kuanza kujibizana na kutupiana maneno na watu ambao wanakupenda na ni wawekezaji wakubwa kwako.

Hao wabunge wajue wanunuzi wakubwa wa mahindi yao, vitunguu na mazao mengine ni hao Wakenya.

Badala yake serikali inajiona ni sifa kuwapiga, kuwateka na kuwabaka wageni au raia yeyote ! Ni bora wangenyamaza.
 
Hahaha wao wanasema mamaa kajenga sgr, shule, kaleta maji, na maisha bora huyo ndiye muwekezaji number moja.
 
Kwahiyo wakiwa wawekezaji ndio watukalie kichwani?

Stupid fish

Watanzania ndio wawekezaji wakubwa zaidi Tanzania
 
Back
Top Bottom