Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Hoja hiyo ilitolewa na Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) na Mussa Mbarouk wa Tanga wakati wakichangia taarifa ya Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo Alhamis Februari 6 2020.
Mbarouk alitoa mfano wa mama aliyemuomba Rais amlipie Sh 5milioni alizokuwa akidaiwa na hospitali ikiwa ni gharama za matibabu kwa mgonjwa wake.
“Maiti wasidaiwe, Kama akifariki ndugu zake wapigiwe simu waje kumchukua ndugu yao na si kumdhalilisha kwa muda mrefu,”amesema.
Naye Sugu amesema Serikali imekuwa ikisema hakuna Mtanzania anayekosa matibabu lakini wanashikilia maiti hospitalini.
Amesema hatua ya kuzuia miili ya waliokufa inawanyima Watanzania wa kwenda kufanya ibada kwa ndugu zao wanaofariki kwa kushindwa kulipia gharama za matibabu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndungulile amejibu hoja hiyo kwa kusema wananchi wanaokosa fedha za kulipia matitabu wanapaswa kwenda kwenye dawati la ustawi wa jamii linalokuwepo katika kila hospitali.
Amesema hawana maiti ambayo wanaishikilia kwa sababu ya madai ya gharama za matibabu kwa sababu ya utaratibu huo.