Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,186
- 7,492
[h=1]Wabunge nchini Kenya wamepiga kura kujiongeza mshahara na kwenda kinyume na tume ya kitaifa ya kuratibitisha mishahara ya maafisa wa serikali.
[/h]
Kura hiyo waliyopiga bungeni hapo Jumanne itawawezesha sasa kupokea mishahara ya dola elfu kumi. Mshahara wa mkenya wa kipato cha kadri ni dola 1,700.
Rais Uhuru Kenyatta aliwaomba wabunge hao mapema mwezi huu kuruhusu mishahara yao kupunguzwa ili waweze kuiwezesha serikali kupata pesa za kutengeza ajira kwa wananchi.
Wabunge wa Kenya ni miongoni mwa wale wanaopokea mishahara mikubwa duniani na hatua yao ya kibinafsi imewaghadhabisha wakenya waliofanya maandamano kuwafananisha wabunge hao na Nguruwe kwa ulafi.
Lakini wabunge hao waliteta kuwa hatua ya kupunguza mishahara yao ni kinyume na sheria.
"wametupokonya utu wetu na lazima tuweze kuurejesha,'' alisema mbunge Jimmy Angwenyi bungeni.
Wabunge katika bunge lililopita walijilimbikizia dola 107,000 kama marupurupu ya kustaafu katika moja ya vikao vyao vya mwisho kabla ya uchaguzi mkuu .
Limeripoti Shirika la Utangazaji la BBC- Leo 29-05-2013.
Swali kwa wadau; Hivi kwa kawaida wanasiasa hujipangia mishahara yao wenyewe?