Wabunge waliomaliza muda hawatakiwi kuitisha mikutano ya hadhara sababu ni raia wa kawaida

Wabunge waliomaliza muda hawatakiwi kuitisha mikutano ya hadhara sababu ni raia wa kawaida

Nahisi hili tamanio lako ni dhidi ya mbunge aliyekuwa wa upinzani. Na kama ni hivyo nadhani unahofia kuona mbunge wa upinzani kupata watu wengi, kwani itaenda kinyume na propaganda yenu kuwa mmeua upinzani.
 
Tuache ushabiki, siasa isitutoe ufahamu, hiyo ndo fact! Unaitisha mkutano kama nani sasa wakati Bunge limevunjwa. Iwe ni TLP, CHADEMA, CCM, CUF, nk.
 
Hapo ujue wanaohofia kuwa tangu wachaguliwe hawajawahi kwenda kwa wapiga kura wao na huko bungeni wamekuwa wakimsifia tu rais bila kusema kero za wapiga kura wao
 
Ubunge ukimalizika kipindi mtu aliyekuwa mbunge haruhusiwi kuitisha mkutano wa hadhara popote sababu ni raia wa kawaida.

Polisi msitoe vibali.
Mbona mawaziri bado wanatoa matamko na wanatumia ofisi na magari ya Serikali nyumba za Serikali kama kawaida wakati siyo wabunge, Ubunge hukoma pindi kampeni ikianza rasmi
 
Hahaha huwa sio vizuri kuondoka bila kuaga.

Watoe vibali sisi Chadema tuwaage wananchi wetu.

Nadhani hata CUF nao walihitaji kuaga wananchi wao sio kampeni, ccm mnaogopa nini?!

Mmejenga madaraja, mmenunua ndege, mmejenga vituo vya afya kila mtaa, mmejenga barabara nchin nzima, dawa mmepeleka hospitali zote kila kata, LAKINI BADO MNAWASIWASI NA WAPINZANI?!

Nilisikia upinzani umekufa mnaogopa nini sasa?!
Muwape vibali waage.
 
Mbona mawaziri bado wanatoa matamko na wanatumia ofisi na magari ya Serikali nyumba za Serikali kama kawaida wakati siyo wabunge, Ubunge hukoma pindi kampeni ikianza rasmi
mzee wale ni part ya serikal bi co wana play part yao kama serikali na sio wabunge
 
Naomba kuuliza hivi..bunge likivunjwa manake wabunge na madiwani wanakua sio wawakilishi tena wa wananchi manake hii inajumuisha spika wa bunge na makamu wake..sasa hao jamaa mbona mpaka sasa wanaitwa majina ya vyeo vyao na gari wanatumia zile zile kabla bunge halijavunjwa..au kuna kitu sikielewi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tuache ushabiki, siasa isitutoe ufahamu, hiyo ndo fact! Unaitisha mkutano kama nani sasa wakati Bunge limevunjwa. Iwe ni TLP, CDM, CCM, CUF, nk.

Hivi tusio wabunge kuna sheria inayotuzuia kufanya mikutano ya hadhara?!
 
Yaani kipindi hiki mataga wote watakatiwa posho yao ya buku saba maana wameonyesha kufeli kazi yao
Nahisi hili tamanio lako ni dhidi ya mbunge aliyekuwa wa upinzani. Na kama ni hivyo nadhani unahofia kuona mbunge wa upinzani kupata watu wengi, kwani itaenda kinyume na propaganda yenu kuwa mmeua upinzani.
 
Mbona mawaziri bado wanatoa matamko na wanatumia ofisi na magari ya Serikali nyumba za Serikali kama kawaida wakati siyo wabunge, Ubunge hukoma pindi kampeni ikianza rasmi
Mawaziri ni serikali na serikali haijavunjwa. Nchi bado ina rais.
 
Back
Top Bottom