MMMMMMMMM!!!!!!!!!!!!
NDUGU HILI NI BUNGE LA NCHI GANI????
MBONA JANA KUNA HOJA ZILIJADILIWA, JE WAILJADILI WAKIWA KWENYE VYUMBANI VYAO???????
AU UILIPIGA PICHA SAA 12:00 ASUBUHI MUDA AMBAO BADO KUFUNGUA MILANGO YA BUNGE???
TUSITEGANE HAPA NA HABARI ZA ULONGO!!!
ANGALIA HII....
Habari za Bunge
‘Wafungwa wanarukishwa kichura gerezani bila nguo'
Imeandikwa na Mwandishi wetu, Dodoma; Tarehe: 1st February 2012 @ 14:05 Imesomwa na watu: 100; Jumla ya maoni: 0
Habari Zaidi:
‘Wafungwa wanarukishwa kichura gerezani bila nguo'
MBUNGE wa Viti Maalumu, Magdalena Sakaya (CUF), amethibitisha mbele ya Bunge kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji akiwa gerezani na kutaka Serikali kuwachukulia hatua wahusika wa vitendo hivyo.
Alisema bungeni hapo kuwa kumekuwapo na vitendo vya wafungwa na mahabusu wa kike kuvuliwa nguo zote na kisha kurushwa kichura chura jambo ambalo ni udhalilishaji mkubwa.
Sakaya aliyasema hayo bungeni jana katika swali lake la nyongeza ambapo alisisitiza kuwa yeye ni shahidi namba moja wa matukio ya udhalilishaji gerezani na iwapo Serikali inataka kumtumia yuko tayari kuthibitisha.
"Ninachojua mimi mfungwa anapoingia gerezani haondolewi haki zake za binadamu, mimi ni shahidi namba moja wa matukio haya, kila siku wafungwa wanavuliwa nguo zote hadi ya mwisho na askari wenzao wa kike huu ni udhalilishaji mkubwa," alisema Sakaya.
Awali katika swali lake la msingi Mbunge wa Viti Maalumu, Mhonga Ruwanywa (Chadema), alitaka kufahamu Serikali itawachukulia adhabu gani polisi wa magereza wanaodhalilisha wafungwa wanawake.
Katika swali lake hilo, alisema kumekuwapo na matukio ya ukatili na uvunjwaji wa haki za binadamu katika magereza nchini likiwamo Gereza la Bangwe katika Manispaa ya Kigoma ambapo alianisha udhalilishaji huo kuwa ni kuvuliwa nguo zote na kuruka kichurachura.
Akijibu maswali hayo yote, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hamis Kagasheki alisema suala hilo la kushtua ndio kwanza Serikali inalisikia kutoka kwa wabunge hao ambapo ilianza kufuatilia katika Gereza la Bangwe, lakini ilishindwa kupata ushahidi.
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!