Wabunge wamegoma kuhudhuria vikao Dodoma

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,925
posho-tupu.jpg

Anaonekana Ana Kilango peke yake, je wabunge wamefanya mgomo kuhudhuria vikao? Pesa zote wanazodai kulipwa ni kwa ajili ya nini kama hawawajibiki katika kuwawakilisha waliowachagua? Hii imetokea February 1, 2012 Dodoma kwenye kikao cha bunge kinachoendelea.
 
Ili kurejesha nidhamu bungeni Mama Makinda anatakiwa kuwachapa viboko akina Sita waisiohudhuria vikao hadi wanashika adabu.
 
posho-tupu.jpg

Anaonekana Ana Kilango peke yake, je wabunge wamefanya mgomo kuhudhuria vikao? Pesa zote wanazodai kulipwa ni kwa ajili ya nini kama hawawajibiki katika kuwawakilisha waliowachagua? Hii imetokea February 1, 2012 Dodoma kwenye kikao cha bunge kinachoendelea.

Mkuu mbunge akishatia saini kitabu cha mahudhurio haitajai kuwepo ukumbini muda wote ila mshiko uko pale pale, sioni tofauti ya mbunge kutokowepo na wale wanaochapa usingizi, hii aibu tunakuomba mheshimiw Rais wetu mpendwa JK aingilia kati hili bunge sasa ni mzigo kwa watanzania na serikali kwaujumla. Matatizo yote yanayolikabili taifamengi yamesababishwa na bunge letu lililojaa mipasho.
 
hivi kama hawapo bungeni watakuwa mitaani au watakuwa wapi''nashindwa kuelewa
 
Ivi sasa watakua wapi manake majimboni kwao ndio awagusi kabisa mpaka uchaguzi ujao kuomba kula,
 
tatizo ni kukosa uzalendo wala sio kweli kuwa hawajui kuwa kazi ya bunge ni wito, kibaya zaidi Taifani/Afrika hatujaigundua elimu hiyo. Sasas mimi naomba kushika mkono ili niibue elimu hiyo na kutegua kitendawili cha kinachoitafuna Afrika si Tanzania tu, yakiwemo mapinduzi ya madaraka dhidi ya mamlaka, ni tayari kuonana na yeyote kwa mahojiano ili tuliokoe Taifa na Bara letu. kwa J4mindu@gmail.com
 
posho-tupu.jpg

Anaonekana Ana Kilango peke yake, je wabunge wamefanya mgomo kuhudhuria vikao? Pesa zote wanazodai kulipwa ni kwa ajili ya nini kama hawawajibiki katika kuwawakilisha waliowachagua? Hii imetokea February 1, 2012 Dodoma kwenye kikao cha bunge kinachoendelea.

MMMMMMMMM!!!!!!!!!!!!

NDUGU HILI NI BUNGE LA NCHI GANI????

MBONA JANA KUNA HOJA ZILIJADILIWA, JE WAILJADILI WAKIWA KWENYE VYUMBANI VYAO???????

AU UILIPIGA PICHA SAA 12:00 ASUBUHI MUDA AMBAO BADO KUFUNGUA MILANGO YA BUNGE???

TUSITEGANE HAPA NA HABARI ZA ULONGO!!!

ANGALIA HII....

Habari za Bunge

‘Wafungwa wanarukishwa kichura gerezani bila nguo’
Imeandikwa na Mwandishi wetu, Dodoma; Tarehe: 1st February 2012 @ 14:05 Imesomwa na watu: 100; Jumla ya maoni: 0

Habari Zaidi:

MBUNGE wa Viti Maalumu, Magdalena Sakaya (CUF), amethibitisha mbele ya Bunge kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji akiwa gerezani na kutaka Serikali kuwachukulia hatua wahusika wa vitendo hivyo.

Alisema bungeni hapo kuwa kumekuwapo na vitendo vya wafungwa na mahabusu wa kike kuvuliwa nguo zote na kisha kurushwa kichura chura jambo ambalo ni udhalilishaji mkubwa.

Sakaya aliyasema hayo bungeni jana katika swali lake la nyongeza ambapo alisisitiza kuwa yeye ni shahidi namba moja wa matukio ya udhalilishaji gerezani na iwapo Serikali inataka kumtumia yuko tayari kuthibitisha.

“Ninachojua mimi mfungwa anapoingia gerezani haondolewi haki zake za binadamu, mimi ni shahidi namba moja wa matukio haya, kila siku wafungwa wanavuliwa nguo zote hadi ya mwisho na askari wenzao wa kike huu ni udhalilishaji mkubwa,” alisema Sakaya.

Awali katika swali lake la msingi Mbunge wa Viti Maalumu, Mhonga Ruwanywa (Chadema), alitaka kufahamu Serikali itawachukulia adhabu gani polisi wa magereza wanaodhalilisha wafungwa wanawake.

Katika swali lake hilo, alisema kumekuwapo na matukio ya ukatili na uvunjwaji wa haki za binadamu katika magereza nchini likiwamo Gereza la Bangwe katika Manispaa ya Kigoma ambapo alianisha udhalilishaji huo kuwa ni kuvuliwa nguo zote na kuruka kichurachura.

Akijibu maswali hayo yote, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hamis Kagasheki alisema suala hilo la kushtua ndio kwanza Serikali inalisikia kutoka kwa wabunge hao ambapo ilianza kufuatilia katika Gereza la Bangwe, lakini ilishindwa kupata ushahidi.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
MMMMMMMMM!!!!!!!!!!!!

NDUGU HILI NI BUNGE LA NCHI GANI????

MBONA JANA KUNA HOJA ZILIJADILIWA, JE WAILJADILI WAKIWA KWENYE VYUMBANI VYAO???????

AU UILIPIGA PICHA SAA 12:00 ASUBUHI MUDA AMBAO BADO KUFUNGUA MILANGO YA BUNGE???

TUSITEGANE HAPA NA HABARI ZA ULONGO!!!

ANGALIA HII....

Habari za Bunge

‘Wafungwa wanarukishwa kichura gerezani bila nguo'
Imeandikwa na Mwandishi wetu, Dodoma; Tarehe: 1st February 2012 @ 14:05 Imesomwa na watu: 100; Jumla ya maoni: 0

Habari Zaidi:

‘Wafungwa wanarukishwa kichura gerezani bila nguo'
MBUNGE wa Viti Maalumu, Magdalena Sakaya (CUF), amethibitisha mbele ya Bunge kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji akiwa gerezani na kutaka Serikali kuwachukulia hatua wahusika wa vitendo hivyo.

Alisema bungeni hapo kuwa kumekuwapo na vitendo vya wafungwa na mahabusu wa kike kuvuliwa nguo zote na kisha kurushwa kichura chura jambo ambalo ni udhalilishaji mkubwa.

Sakaya aliyasema hayo bungeni jana katika swali lake la nyongeza ambapo alisisitiza kuwa yeye ni shahidi namba moja wa matukio ya udhalilishaji gerezani na iwapo Serikali inataka kumtumia yuko tayari kuthibitisha.

"Ninachojua mimi mfungwa anapoingia gerezani haondolewi haki zake za binadamu, mimi ni shahidi namba moja wa matukio haya, kila siku wafungwa wanavuliwa nguo zote hadi ya mwisho na askari wenzao wa kike huu ni udhalilishaji mkubwa," alisema Sakaya.

Awali katika swali lake la msingi Mbunge wa Viti Maalumu, Mhonga Ruwanywa (Chadema), alitaka kufahamu Serikali itawachukulia adhabu gani polisi wa magereza wanaodhalilisha wafungwa wanawake.

Katika swali lake hilo, alisema kumekuwapo na matukio ya ukatili na uvunjwaji wa haki za binadamu katika magereza nchini likiwamo Gereza la Bangwe katika Manispaa ya Kigoma ambapo alianisha udhalilishaji huo kuwa ni kuvuliwa nguo zote na kuruka kichurachura.

Akijibu maswali hayo yote, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hamis Kagasheki alisema suala hilo la kushtua ndio kwanza Serikali inalisikia kutoka kwa wabunge hao ambapo ilianza kufuatilia katika Gereza la Bangwe, lakini ilishindwa kupata ushahidi.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

Wabunge wanakawaida ya kuingia asubuhi kuweka sahihi ya mahudhurio kisha wanasepa kwenye mambo yao. Hii picha ni katika moja ya vikao vya siku hiyo sehemu hiyo anaonekana huyu mama peke yake. Labda unajenga utetezi wako huenda we ni mmojawapo wa wabunge walioacha kiti wazi katika kkao hicho.
 
KUNA COMPUTER kali siku hizi labda mpiga picha ka-edit , kama ni kweli inabidi hata 70 ipunguzwe hadi 40
 
Wabunge wanakawaida ya kuingia asubuhi kuweka sahihi ya mahudhurio kisha wanasepa kwenye mambo yao. Hii picha ni katika moja ya vikao vya siku hiyo sehemu hiyo anaonekana huyu mama peke yake. Labda unajenga utetezi wako huenda we ni mmojawapo wa wabunge walioacha kiti wazi katika kkao hicho.

Kweli tupu, wabunge wengi wanaingia jamii forums, na wanaopinga hoja hii ndio wanaoachia viti wazi wako kwanye mahoteli, mabaa na kwenye starehe nyingine wakai vikao vinaendelea wakijua posho zinaingia. Umeona wanavyotetea kwa nguvu zote kuhusu posho bila haya wakati jamii ya watanzania ipo kinyume na posho hizo.
 
Mkuu mbunge akishatia saini kitabu cha mahudhurio haitajai kuwepo ukumbini muda wote ila mshiko uko pale pale, sioni tofauti ya mbunge kutokowepo na wale wanaochapa usingizi, hii aibu tunakuomba mheshimiw Rais wetu mpendwa JK aingilia kati hili bunge sasa ni mzigo kwa watanzania na serikali kwaujumla. Matatizo yote yanayolikabili taifamengi yamesababishwa na bunge letu lililojaa mipasho.

Ilikuwa nikubonyezee LIKE lakini hapo penye bold pamenichefua!!!
 
Back
Top Bottom