Wabunge wamekuwa walalamishi bila kutoa ushauri

Wabunge wamekuwa walalamishi bila kutoa ushauri

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Wabunge wengi badala ya kutafuta suluhisho la mfumuko wa bei wanatafuta kiki tu.

Tumemsikia Gambo na Bushiru wote wana lalamika na kuuliza maswali wakati waziri wa kilimo alishajibu tena kwa upana wake.

Badala ya kulalama watoe suluhisho mfano

1. Je wanafikiri ruzuku iongezwe na pesa itoke wapi? wasije tena wakalaumu matumizi ya pesa

2. Je mnataka kuzuiwe uuzaji wa mazao nje na kuwafanya wawekezaji wa kilimo na wakulima kupata hasara. Je msimu ujao wakiacha kulima hawa wabunge watakuwepo kwenye lawama?

3. Je ruzuku ya mafuta iongezwe na pesa itoke kwenye mradi gani? Isije tena hao hao wabunge waka lalamika deni la nchi kuongezeka hasa kama serikali ikiamua kukopa

Ni rahisi kukaa na kulalamika lakini wabunge wanatakiwa kupendekeza suluhisho na kuwa na uwezo wa kubeba lawama.

Badala yake wanauliza maswali ambayo tayari yana majibu. Na kama hawana data basi wangeulizia data kabla ya kikao cha bunge.

Ukisikiliza vizuri wabunge wengi hawatoe hoja za suluhisho kwasababu hawana suluhisho ambalo serikali halijafanyia kazi. Nimefuatilia sana wizara ya kilimo na Bashe anafanya kitu kitu kama inavyotakiwa

Zitto , Pascal Mayalla ,

Mfano huyu Dr wazo gani katoa zaidi ya kuuliza maswali ambayo Bashe alisha jibu kwenye press ikulu

Uwezo haupo,kwani kupatwa kwao ni afadhali ya kupatwa kwa mwezi🤔
 
Kuanzia Rais analalamika.
Makamu wa Rais analalamika.
Katibu mkuu kiongozi analalamika
Waziri mkuu analalamika
Mbunge analalamika
Mkurugenzi analalamika
Meneja analalamika.

Mfano Waziri wa Kilimo anasema mbolea ipo ya kutosha hapa kigoma, na wakulima wauziwe kwa bei elekezi.

Mkulima wa kigoma, Mimi nasikia tu kuna mbolea ya ruzuku, nimepanga mstari hapa lakini anayetoa mbolea, afisa kilimo anasema bado wanahakiki na hawajapewa bei elekezi.

Rais anatembelea kigoma, anakutana na kero ya kukosekana kwa mbolea, mara utasikia, nilishaleta mbolea lakini blahblah kibao, nitamwambia waziri alitizame na hili.

Mbunge wa Kigoma, Ndalichako anarudi jimboni naye utasikia, hili tatizo nimelipata naona hakuna uwazi, nitalipeleka kwa Rais.

Rais, nimelipokea nimempa mwongozo waziri wa kilimo.

Waziri wa kilimo, hawa watendaji wa kilimo nawapeleka sehemu husika na habari hii itafika kwa Rais ili wafukuzwe kazi, sababu wanaiba mbolea ya wakulima.

Yaani ni kulalamika tu.
 
Kutumaini viongozi wa aina hii ni kujilisha upepo tu.
 
Serikali sikivu ndio msemo wao wakutupumbaza watanzania
 
Back
Top Bottom