Wabunge wamevuka mto kichawi kwa kuruka na ungo, harafu wanarudi nyuma kujenga daraja!!

Wabunge wamevuka mto kichawi kwa kuruka na ungo, harafu wanarudi nyuma kujenga daraja!!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Mkataba staili ya MANGUNGO unawasuta!! Dhamiri zinawasuta!! Wanakula lakini hawashibi!! wanacheka lakini hawana furaha!!! KISA: Watanzania wamewagundua walivyoridhia mkataba wa kuuza bandari zetu kwa bei ya bure tena kinyume kabisa na sheria zetu zilizopo!!

Sasa wanajipanga kurekebisha sheria iliyokiukwa ili ikubaliane na uuzwaji wa rasilimali zetu!! Yaani wamevuka kichawi mto kwa kuruka na UNGO, na sasa wanataka kurudi nyuma na kujenga daraja ili kuficha uchawi wao wa kuruka na UNGO hasa kwa vizazi vijavyo!! Ili watu waje kuona kuwa walivuka kwa daraja!!

Tuukaliane tu kuwaita hawa wabunge ni MANGUNGOS wa kizazi kipya!!
 
Ujinga wao mkubwa ni kwamba hawajui hizo sheria zilitungwa ili kulinda rasilimali zetu na mkataba wowote unaokinzana na sheria hzo maana yake una nia ovu ya kuiba au kunyonya rasilimali za nchi yetu
 
Tuliaaaa upooo? Utawadanganya watu wote lakini huwezi kuidanganya dhamiri yako!!!! Bunge limefanya kituko na fedheha likiwa chini yako!!! Utakuwa mgeni wa nani??
 
Kwa lugha ya kitaalamu tunaweza kusema wamejipakata
 
Eti kiongozi wao ndiye anataka nafasi ya uraisi IPU , pumbavu zake. Tutawaambia wajumbe wa IPU ujinga wote anaoufanya kwenye vikao vyao.
 
Ujinga wao mkubwa ni kwamba hawajui hizo sheria zilitungwa ili kulinda rasilimali zetu na mkataba wowote unaokinzana na sheria hzo maana yake una nia ovu ya kuiba au kunyonya rasilimali za nchi yetu
Lile liprofessor la majalalani , lile linalofyatua mimacho kama jehu nadhani litabaki kadastree kadastree nchi inauzwa.
 
Bunge na Serikali wamejichafua sana ,kwasasa tunasubiri muhimili mmoja tu Mahakama kutenda haki kwenye kesi ya Boniface.
 
Ujinga wao mkubwa ni kwamba hawajui hizo sheria zilitungwa ili kulinda rasilimali zetu na mkataba wowote unaokinzana na sheria hzo maana yake una nia ovu ya kuiba au kunyonya rasilimali za nchi yetu
Jah People
Msukuma
Kibajaji and the likes
 
Halafu huwezi kuamini CCMbila aibu wamejipanga kusukuma mbele huu uuzaji wa bandari zetu kwa nguvu zote kupitia vikao vyao vya kamati kuu na halmashjauri kuu, Eti wanaiagiza serikali iwaelimishe manufaa ya huu mkataba wa staili yaMANGUNGO! Nilisoma habari zao kwenye gazeti la uhuru mpaka nikapata kichefuchefu!!
 
Back
Top Bottom