Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) na Kamati ya Bajeti ya Bunge pamoja na wabunge mbalimbali wamezungumzia maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam, yanayotekelezwa na Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kusifia maendeleo yake ikiwa ni pamoja na uamuzi wa kumleta mwekezaji binafsi, DP World.
Kwa mujibu wa taarifa ya PIC, mradi huo unatekelezwa kwa awamu mbili; awamu ya kwanza inahusisha upanuzi wa gati kuanzia namba 7 hadi 11, na ulianza kutekelezwa mwaka 2017 na ulitarajiwa kukamilika mwaka 2024. Awamu ya pili, ambayo inahusisha ujenzi wa gati 12 hadi 15, inatarajiwa kufanyika baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza.
Soma Pia: Prof Kitila: Waliopinga DP World Wakiri Mafanikio Yake Hadharani
Aidha Wakichangia taarifa ya kamati hiyo ya PIC na ile ya Bajeti wabunge wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan na serikali yake kwa kuziba masikio kuhusu suala la kuleta mwekezaji, DP World kuendesha sehemu ya bandari, hatua baadhi ya watu walijitahidi kupotosha ukweli kuhusu mwekezaji huyo. Wabunge wamesema ongezeko la mapato limechangiwa sana na ujio wa DP World.