Wabunge wanaodemka hawajui machungu ya kutafuta kura

Wabunge wanaodemka hawajui machungu ya kutafuta kura

MC44

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2019
Posts
2,169
Reaction score
3,297
Tangu Bunge jipya kuanza kumekuwa na vihoja na viroja kutoka bungeni nadhani hii ni kwa sababu wabunge wengi wapo pale kwa hisani ya mtu.

Wengine ndo hao viti maalum. Hawajui haso za kusaka kura mitaani.

Hawajui wakiwa bungeni ni kujipigia kampeni ili akija mtaani asitumie nguvu nyingi sana ukizingatia watz wengi wanatumia vyombo vya habari na wanafuatilia vyema.

Mimi nipo jimbo fulani najua mbunge wangu pia hujawahi kuzungumza chochote na tunajua ulienda kwa hisani ya mwendazake.

Majimbo yapo 169 hivi lakini tuna wabunge 400's zaidi ya nusu ni MAMLUKI.

Katiba iangalie tena. Bado kuna wale wasokuwa na chama (19) wapo tu.

Haya vijana dhaifu naona wamesemewa upungufu wa nguvu za kiume na mwanamama wa viti maalum maana ndo matatizo ya jimbo lake hilo lisilojulikana.

Akija kuomba kura mtampa Kwani kawatetea.

Any way Kuna mdundo mzuri sana unarindimba kutoka humu, nasubiri kuona wademkaji wetu katika ubora wao.
 
Majimbo yapo 169 hv lkn tuna wabunge 400's zaidi ya nusu ni MAMLUKI.
Katiba iangalie tena
Bado kuna wale wasokuwa na chama (19) wapo tuu.....
mhhhhhhhhhhh.

Uzi una takataka hizo nilizowekea rangi nyeusi ya kukoza, hebu rudi kwenye makabrasha yako Kisha uje usafishe uchafu wako.
 
Jambo la kujiuliza je Wabunge wamekuwa wakimlinganisha Mwendazake na Mrithi wake? Au wamechukua hatua kuzima njama zilizokuwa zime andaliwa za kumchafua mwendazake.

Wabunge bado wanao nafasi ya kuendelea kuisimamia serikali na kulipa heshima yake inayostahili Bunge. Watafanikisha hili kwa kuendelea na kuonesha kuwa ni lazima na si hiari kutunza heshima ya mwendazake anayioistahili na aliyoitolea jasho kwa kuwa mtumishi wa wananchi. Kuwa onesha wote wenye njama za makusudi na hila ya kuichafua legacy hiyo kuwa hawatafanikiwa kamwe.

Uzuri wenyewe Bunge linao wajibu wa kuisimamia serikali na kufanikisha utendaji wake. Wafanyekazi hiyo kwa uadilifu, kweli na haki yote. Watajijengea heshima na hakuna atakaye thubutu tena kuwaita majina ya ajabu.
 
Mdemkaji Mkuu ni Majaliwa akisaidiwa na Ndugai
 
Wameambiwa waache kudemka... kisha kwa wingi wao wakainuka kudemka![emoji40]
 
Back
Top Bottom