Wabunge Wanawake Zanzibar: Uwekezaji Unaofanywa Umekuwa Kichocheo cha Kukuza Uchumi Zanzibar

Wabunge Wanawake Zanzibar: Uwekezaji Unaofanywa Umekuwa Kichocheo cha Kukuza Uchumi Zanzibar

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WABUNGE WANAWAKE ZANZIBAR: UWEKEZAJI UNAOFANYWA UMEKUWA KICHOCHEO CHA KUKUZA UCHUMI ZANZIBAR

Wakiwa Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 30 Novemba, 2024, Wabunge Wanawake Zanzibar wameeleza kuwa Uwekezaji unaofanywa na Serikali umekua ni kichocheo cha kukuza uchumi na maendeleo ya nchi.

Hayo yamesemwa na Wabunge wa Viti Maalum na Wabunge wa Majimbo wakati wakihitimisha ziara ya kuangalia Miradi ya maendeleo iliyofanywa na Serikali ya awamu ya nane kwa upande wa Mkoa wa kusini Unguja ambapo Uwekezaji umezidisha ajira kwa Wananchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe. Ayoub Muhammed Mahmoud amewapongeza Wabunge Wanawake Zanzibar kwa kufanya ziara ya kuangalia miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa wa Kusini Unguja jambo ambalo limeweza kuwapa faraja.

Ayoub Muhammad Mahmoud Amesema kuwa Serikali zote mbili za Tanzania, zimefanya mambo mengi mazuri ya kutatua changamoto za Wananchi na kutengeneza fursa mbalimbali za kijamii, kiuchumi, kisiasa na kimaendeleo na kuzidi kutatua changamoto nyingi zilizokuwa zinawakabili wanachi

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Kati, Mhe. Gallos Nyimbo na Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja, Mhe. Othman Ali Maulid Waliposhiriki katika ziara hiyo, wameelezea kufarijika kwao kutokana na ziara ya Viongozi hao na kuahidi kushirikiana ili kufikia malengo yaliyopangwa na Serikali.

Vilevile, viongozi wa Serikali Kusini Unguja wameahidi kusimamia miradi yote ya Serikali ili iweze kuwa endelevu na kuwaletea maendeleo Wananchi na kuleta tija na kunyanyua Uchumi kwa mtu mmoja mmoja na uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Ziara ya siku tatu ya kutembelea miradi ya kimaendeleo ilianzia Mkoa wa Mjini Magharib, Kusini Unguja na Mkoa wa Kaskazini Unguja iliyojumuisha Wabunge wa Viti Maalum na Wabunge wa Majimbo kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vya upinzani Zanzibar.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-12-02 at 09.49.49.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-02 at 09.49.49.jpeg
    209.3 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-12-02 at 09.49.52 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-02 at 09.49.52 (1).jpeg
    504 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-12-02 at 09.50.03 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-02 at 09.50.03 (1).jpeg
    425.7 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-12-02 at 09.50.03.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-02 at 09.50.03.jpeg
    575.2 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-12-02 at 09.49.55 (4).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-02 at 09.49.55 (4).jpeg
    197.4 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-12-02 at 09.49.55.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-02 at 09.49.55.jpeg
    453.4 KB · Views: 6
Back
Top Bottom