Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Wabunge wa Umoja wa Wanawake (UWT) Zanzibar (Wabunge wa Majimbo na Wabunge wa Viti Maalum) tarehe 28 Novemba, 2024 wameanza ziara rasmi kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Rais, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Katika ziara yao, Wabunge Wanawake Zanzibar wameeleza kuwa Kutekelezwa kwa miradi mikubwa ya kimkakati na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kumesaidia sana kuleta maendeleo kwa wananchi wa maeneo hayo ambapo miradi inatekelezwa na kuweka urahisi wa utoaji huduma kwenye jamii.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ziara ya Wabunge wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Tanzania kutoka Zanzibar katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwanduwi, Katibu wa Idara ya Itikadi, Siasa, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Khamis Mbetto Khamis Amesema miradi hiyo ni pamoja na Barabara, Masoko, Elimu, Afya na Michezo.
Khamis Mbetto Khamis. Amesema kuwa maendeleo makubwa Zanzibar yamepatikana kupitia miradi ikiwemo kuzalisha ajira kwa vijana na kustawisha uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kw ujumla.
Khamis Mbetto Khamis Amefahamisha kuwa kazi kubwa imefanywa na viongozi waliopo madarakani kwa kuhakikisha kuwa wanasogeza huduma za muhimu kuwa karibu na Wananchi wao.
Aidha, Khamis Mbetto Khamis Amesema kutekelezwa kwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 kwa vitendo kumesaidia kutengeneza matumaini kwa wananchi pamoja na kukiwezeaha Chama Cha Mapinduzi kuendelea kushinda katika chaguzi.
Naye, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania-UWT (Zanzibar) Ndugu Tunu Juma Kondo amesema ziara ya Wabunge Wanawake imeleta tija sambamba na kutangaza maendeleo yaliyopatikana katika kipindi chote cha Uongozi wa Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa amesema kuwa katika kuhakikisha Mkoa wa Mjini Magharibi unabaki salama, Jeshi la Polisi linaendelea kufanya Operesheni maalum ya Ondoa Uhalifu ili Wananchi waendelee kuishi kwa Amani na Utulivu.
Vilevile, pamoja na mambo mengine Wabunge Wanawake Zanzibar wamesifu maendeleo yaliyopatikana katika Sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Afya, Elimu na Miundombinu ya Barabara kwani yamechangia kwa kiasi kikubwa kuzalisha ajira.
Ziara ya Wabunge Wanawake Zanzibar imeanzia Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Forodhani, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Lumumba, Skuli ya Tumekuja, Kituo kipya cha Daladala, Soko la Jumbi na Mwanakwerekwe, Mradi wa Maji Dole, Mradi wa Soko la Nyanya na Nungwi.
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-11-29 at 10.52.20.jpeg298.6 KB · Views: 2 -
WhatsApp Image 2024-11-29 at 10.52.18.jpeg292.5 KB · Views: 2 -
WhatsApp Image 2024-11-29 at 15.50.14.jpeg245.1 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-11-29 at 10.50.39.jpeg322.2 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-11-29 at 10.50.25.jpeg356.3 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-11-29 at 15.52.08.jpeg331.1 KB · Views: 3