Wabunge wanne - Anthony Komu, Joseph Selasini, David Silinde na Wilfred Lwakatare wafutwa uanachama wa CHADEMA

Wabunge wanne - Anthony Komu, Joseph Selasini, David Silinde na Wilfred Lwakatare wafutwa uanachama wa CHADEMA

Ni makosa makubwa kuendelea kuamini kwenye maisha kwamba watu wote unaoweza kufanya nao urafiki wasiwe wasaliti, Eti watu wote ambao unaweza kujenga nao Chama kusiwemo wasaliti!! Huo ni Ujinga mkubwa,

kuondoa usaliti mahali popote, ni meza huru isiyo na vitisho,

Watu Wana chalenji habari za Mungu sembuse Vyama ambavyo watu wake ni wale wenye kutumia akiri na Wakati wowote makosa hujitokeza, unategemea kusitokee usaliti

Na usaliti mwingine husababishwa na mwenye nyumba, pindi anapokosa busara na kuendekeza maamuzi ya mabavu,
point..... ila ujashauri Mkuu nini kifanyike au kilichofanywa ni sahihi?
 
Chama cha Mtu na Mkwewe, leta Fyoko wanaku-fyokoa, 😂😂😂😂 Mwenyekiti wa Kudumu hataki mchezo... Siasa bana.
 
Kikao cha kamati kuu ya Chadema kilichoongozwa na mwenyekiti wake mh Mbowe kwa njia ya mtandao kimefanya maamuzi magumu mno.

Taarifa ya maamuzi hayo inategemewa kutolewa leo na Katibu Mkuu wa chama hicho Mh. John J. Mnyika.

—————
UPDATES
—————
Akitolea maamuzi hayo, Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema

Kamati Kuu CHADEMA imeazimia Wabunge Anthony Komu na Joseph Selasini pamoja na kuwa wamejipotezea sifa ya uanachama wa CHADEMA, wameendelea kutoka kauli za kejeli, kashfa na kukiuka maagizo ya Chama, hivyo Chama kimeazimia kuwafukuza uanachama

Mbunge David Silinde na Wilfred Rwakatare sio tu wamekiuka agizo la Chama bali wamekuwa wakijitokeza kwenye vyombo vya habari kutoa maneno ya kashfa na kejeli dhidi ya maagizo ya Chama na Viongozi wa Chama, Kamati Kuu CHADEMA imefikia uamuzi wa kuwafuta uanachama.

Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Mariamu Msabaha, ameshiriki kukiuka maagizo ya Chama, ilitakiwa awe mfano na kwakuwa amekwenda kinyume, amevuliwa nafasi zake zote ndani ya Chama na kubaki na Ubunge na atatakiwa ajieleze kwanini asichukuliwe hatua zaidi kwa kukiuka maagizo.

View attachment 1447012
View attachment 1447013
View attachment 1447014
Kiongozi; Na hii ndio siasa. Waumini; Tumshukuru Mungu.
 
Wafukuzwe tu uanahaihitajina kukiuka maamuzi mliokubaliana ni usaliti tosha haihitaji elimu kubwa kutambua usaliti kama huo
 
Wangetangaza kujiondoa kwenye uchaguzi mkuu kabisa ili waendelee kukaa karantini.
Mnataka Jiwe asiwe na mpinzani kugombea Urais kwa sababu hawezi kufanya kampeni afya yake mbaya? Simamisheni mgombea asiyekuwa na mgogoro na afya yake!
 
Back
Top Bottom