mwaswast
JF-Expert Member
- May 12, 2014
- 12,780
- 6,480
Mbunge wa jimbo la Singida Magharibi kwa kupitia chama cha mapinduzi Ndugu Elibariki Emmanuel Kingu Leo amepigana na mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika jimbo la Mfenesini Ndugu Othman Said Machano Cairo Misri.
Fedhehea hiyo ya nchi imetokea katika hoteli ya Radisson mjini Cairo, Baada ya Mbunge Kingu kumtolea Maneno ya Kashfa Mhe Machano wakati wa kikao cha wabunge walioenda kuiwakilisha nchi yetu Katika kombe la AFCON 2019 ambayo yanafanyika Misri.
Baada Bw Kingu kumtolea maneno haitoshi alisimama na kumkata mtama, Ndipo Mbunge wa viti maalum wa Chadema akiwakilisha Zanzibar Mhe Mariam Msabaha kusimama na kuamulia nae akapigwa Ngumi ya uso kutoka kwa Bw Kingu.
Ndipo askari polisi kutoka Misri alipoamua kuingilia kati na kumtuliza bw kingu, Akiongea mmoja wa wahudumu wa Hoteli huyo alisema "Watanzania Ambao tuliokuwa tunawasikia wanapendana ndio hawa kwa hapa wameonyesha kutokuwa wastaarabu kabisa na wamesababisha kuwapigia kelele wateja wetu.
Kitendo hiki kimetokea Leo Mchana hii ni Aibu sisi kama taifa kingu ametuaibisha sana, ametutia aibu na kuitia Nuksi timu yetu ya Taifa.
C&P