Tetesi: Wabunge washauri Luhaga Mpina afukuzwe CCM

Tetesi: Wabunge washauri Luhaga Mpina afukuzwe CCM

Wabunge kadhaa wamedaiwa kupeleka malalamiko kwa Rais Samia kwamba Luhaga Mpina afukuzwe CCM kutokana na kile wanachodai kukiharibu Chama cha Mapinduzi mbele ya watanzania.

Wabunge wanaotajwa kumchongea Mpina kwa Rais ni Wajumbe NEC wakiongozwa na Livingstone Lusinde, Joseph Kasheku Msukuma, Januari Makamba, Mwigulu Nchemba, Hussein Bashe, Makame Mbarawa.

Wabunge hao wanatajwa kuendesha kampeni za chini kwa chini na kumshauri Mama amfukuze Mpina CCM. Tusubiri tuone CCM ni dude kubwa.
nadhani ni muhimu zoezi hili likafanyika mapema zaidi bila kubabaika wala kuchelewa, mtu huyu ameshakosa sifa na weledi wa kua mwanachama wa ccm.

aondolewe haraka ili akapate muda wa kutosha na fursa nzuri zaidi ya kuinanga ccm akiwa huko kwa mapanya rodi...
 
Kumbe habari ya muda!
 
Wabunge wanaotajwa kumchongea Mpina kwa Rais ni Wajumbe NEC wakiongozwa na Livingstone Lusinde, Joseph Kasheku Msukuma, Januari Makamba, Mwigulu Nchemba, Hussein Bashe, Makame Mbarawa.
Mpina shikilia hapo hapo wameanza kuruka na kukanyagana,
hebu ibuka na ile ya vigogo kununua nyumba Osterbay na Masaki najua Mwingulu, January, Mbarawa hawakosi kweny hiyo list of shame!!
 
Kwa hiyo ile Demokrasia inayodaiwa kukua sana awamu hii ni ipi hasa kama kuhoji tu bado ni kosa!
 
Ukiangalia list ya hao wabunge, ni wale wanufaika wa DP WORLD.
Tatizo la Ccm hawa taki msema kweli.
Mwigulu, Mbarawa, wana tajwa sana kwenye rushwa na kuji limbikizia mali.
Mama kalogwa hasikii wala haoni juu ya hawa wezi.
Ninge kuwa mimi Mh Rais ningebmteua Mpina kwenye nafasi za mmoja wao.
Kwa kimya cha Mama tuna fikiria kusema na yeye ni mnufaika wa yanayo endelea.
Msukuma rudisha V8 uliyo hongwa na Waarabu.
Makamba ndie huyo ali wekwa kwenye Nishati shida ya umems tuna iona hadi leo. Bado Rais ana mbadilishia wizara. Tusemeje kuhusu huyu Rais?? Hana huruma na Watanzania kabisa.
Siyo kalogwa huyo bibi naye ni mwizi tuu, inakuwaje watu wanaiba wewe upo kimya?
 
Walau yeye anapasua ukweli kuliko wale wanaojikombakomba ili wapewe nafasi!
Hata yeye anajikomba kimtindo huwajui vizuri hao wakitakaga nafasi hutumia mbinu hiyo yaani kila kukicha ni kukosoa tu ikitokea hivyo wenyewe wanajuana kwamba jamaa ana kiu ya asali wacha tumlambishe kidogo basi anapoa anakuwa mzee wa mapambio kazi inakuwa ni kusifu na kuabudu basi.
 
Kwahiyo unataka kuniambia Bashe pia alikuwa mkali sana bungeni kabla ya kulambishwa u naibu waziri? 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Wabunge kadhaa wamedaiwa kupeleka malalamiko kwa Rais Samia kwamba Luhaga Mpina afukuzwe CCM kutokana na kile wanachodai kukiharibu Chama cha Mapinduzi mbele ya Watanzania.

Wabunge wanaotajwa kumchongea Mpina kwa Rais ni Wajumbe NEC wakiongozwa na Livingstone Lusinde, Joseph Kasheku Msukuma, Januari Makamba, Mwigulu Nchemba, Hussein Bashe, Makame Mbarawa.

Wabunge hao wanatajwa kuendesha kampeni za chini kwa chini na kumshauri Mama amfukuze Mpina CCM. Tusubiri tuone CCM ni dude kubwa.
Itakuwa mwanzo wa Taharuki ndani ya CCM hasa ikizingatiwa Mh Mpina amekuwa akionekana mzalendo kwa wabTz wengi hili laweza kuwa jaribio baya kabisa
 
Back
Top Bottom