Natumai hapa tunajaribu kujifaji na impossibilities.
Ila kama ni jambo la kutolea maoni mimi binafsi sioni logic ya wabunge viti maalum.
Ni kweli ndani ya hivi viti maalumu kuna wapambanaji walioonyesha dhahiri uwezo wao na nia ya dhati ya kutetea maslahi ya Taifa na raia zake. Hao ndio nafikiri wangefikiriwa na vyama vyao kuachiwa majimbo wanakotoka wasimame kama wagombea.
Ama katika mabadiliko ya katiba, napendekeza nafasi ya wabunge wa kuteuliwa kwa chama kitakachoongoza ziwe ni 20 na kambi ya upizani viti 10. Hizi nafasi zote ziwe ni kwa wanawake tu, ili kuweza kuwarudisha wale kina mama wa shoka bungeni.
.