Wabunge wasomi endeleeni kuchutama. Msijibishane na wa darasa la saba

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Ni kawaida kwa mtu mwenye akili zake (muungwana) akianza kurushiwa maneno na kichaa huwa anakaa kimya.

Vivyo hivyo muungwana akiporwa nguo zake na kichaa, huwa anachutama.

Sasa wabunge darasa la saba kwasababu ya upeo wao finyu, hubwatuka tu dhidi ya wabunge wasomi wenye akili. Na wabunge hawa wasomi huamua kutulia tu ( huchutama).

Kwasababu ya ukimya utokanao na busara za hawa wabunge wasomi, wale wa darasa la saba kwa ujinga wao huona kama wanapendwa na hivyo wana "madini" ya kutosha.

Umma unafuatilia mijadala bungeni, lkn bahati mbaya kila siku umma unakutana na mipasho/matusi ya wabunge darasa la saba. Wanainanga elimu na kuwatweza wasomi. Wanautukuza ujinga na udarasa la saba.

Kuna haja ya kubadilisha sifa ya mtu kugombea ubunge. Ili iwe walau shahada ya kwanza, kw lengo la kuwaondoa hawa vichaa wa darasa la saba.
 
Bunge hili hata akina babu Tale wametinga..
Kweli ukishangaa ya Musa utaona ya Firauna
Yote haya ni makosa yasiyo sameheka ya mwendazake. Alivuruga uchaguzi vichaa wa ccm wakapewa ushindi.
 
Mkuu kuna bifu za wazi kabisa sio bungeni hata mitaani watu walio kimbia umande huwananga vibaya sana watu walio soma
Tunaliharibu taifa. Watoto wetu wakiyasikia haya kwa watu wenye rank ya ubunge hawatasoma.

Bila Shaka hata hawa wa mitaani wameathiriwa na akina Lusinde na Msukuma.
 
Lusinde na Msukuma waende veta waziri mkuu katangaza nafasi za masomo
 
1618693401112.jpeg
 
Ningekuwa Ndugai huyu Lusinde na Musukuma wasingekuwepo bungeni. Wanatoa Picha mbaya sana kwa Taifa linalijitafutia maendeleo kwa jitihada mbalimbali ikiwemo Elimu. Hata kama hao walioko bungeni wamefunika akili na kufunua matumbo itoshe tu wao kina Musukuma kutambua si wote wamejivua nguo kama Kabudi na Kimei. Waheshimu taaluma maana watajuta siku moja
 
Ni kawaida kwa mtu mwenye akili zake (muungwana) akianza kurushiwa maneno na kichaa huwa anakaa kimya.

Vivyo hivyo muungwana akiporwa nguo zake na kichaa, huwa anachutama.

Sasa wabunge darasa la saba kwasbb ya upeo wao finyu, hubwatuka tu dhidi ya wabunge wasomi wenye akili. Na wabunge hawa wasomi huamua kutulia tu ( huchutama).

Kwasbb ya ukimya utokanao na busara za hawa wabunge wasomi, wale wa darasa la saba kwa ujinga wao huona kama wanapendwa na hivyo wana "madini" ya kutosha.

Umma unafuatilia mijadala bungeni, lkn bahati mbaya kila siku umma unakutana na mipasho/matusi ya wabunge darasa la saba. Wanainanga elimu na kuwatweza wasomi. Wanautukuza ujinga na udarasa la saba.

Kuna haja ya kubadilisha sifa ya mtu kugombea ubunge. Ili iwe walau shahada ya kwanza, kw lengo la kuwaondoa hawa vichaa wa darasa la saba.
as long as ccm iko madarakani kubadili vigezo vya elimu inakuwa ngumu
 
Ni kawaida kwa mtu mwenye akili zake (muungwana) akianza kurushiwa maneno na kichaa huwa anakaa kimya.

Vivyo hivyo muungwana akiporwa nguo zake na kichaa, huwa anachutama.

Sasa wabunge darasa la saba kwasababu ya upeo wao finyu, hubwatuka tu dhidi ya wabunge wasomi wenye akili. Na wabunge hawa wasomi huamua kutulia tu ( huchutama).

Kwasababu ya ukimya utokanao na busara za hawa wabunge wasomi, wale wa darasa la saba kwa ujinga wao huona kama wanapendwa na hivyo wana "madini" ya kutosha.

Umma unafuatilia mijadala bungeni, lkn bahati mbaya kila siku umma unakutana na mipasho/matusi ya wabunge darasa la saba. Wanainanga elimu na kuwatweza wasomi. Wanautukuza ujinga na udarasa la saba.

Kuna haja ya kubadilisha sifa ya mtu kugombea ubunge. Ili iwe walau shahada ya kwanza, kw lengo la kuwaondoa hawa vichaa wa darasa la saba.
Mkuu nimecheka kwa nguvu mbele za watu,ETI WANA MADINI YA KUTOSHA.
IMG-20210417-WA0009.jpg
 
CCM imewekeza Sana kwenye ujinga ndiyo maana inakumbatia Sana wajinga
Nimeona hata Kule chato jamaa wamewekewa mpaka uwanja Wa ndege,ofisi Kali ya TRA,CRDB nk,

Lakini elimu bora hawakuekezewa.
 
Ndhani kuanzia Sasa uwanja wa ndege utageuka kuwa machungio ya ng'ombe. Hayo maofisi yakuwa madarasa ya chekechea.
 
Ningekuwa Ndugai huyu Lusinde na Musukuma wasingekuwepo bungeni. Wanatoa Picha mbaya sana kwa Taifa linalijitafutia maendeleo kwa jitihada mbalimbali ikiwemo Elimu. Hata kama hao walioko bungeni wamefunika akili na kufunua matumbo itoshe tu wao kina Musukuma kutambua si wote wamejivua nguo kama Kabudi na Kimei. Waheshimu taaluma maana watajuta siku moja
Unamzungumzia Ndugai yupi? Huyu huyu anayewapongeza hao La Saba kuwa wanajenga hoja vizuri? We ushangai kila siku wanapata nafasi ya kuongea bungeni?

Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
 
Ndhani kuanzia Sasa uwanja wa ndege utageuka kuwa machungio ya ng'ombe. Hayo maofisi yakuwa madarasa ya chekechea.
majeshi yetu hayana viwanja vya ndege vvya kutosha,ukiacha ngerengere vingine vyote wanatumia vya kiraia, mfano mwanza huohuo wa kiraia unatumika na jeshi pia,mtizame mbali zaidi ya kuchungia ngombe wapewe jeshi la wananchi.
 
Back
Top Bottom