Wabunge, Wawakilishi na wajumbe wa Bunge la Katiba wapongeza msimamo wa Kanisa Katoliki.

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Posts
5,536
Reaction score
2,266
WABUNGE na Wawakilishi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamepongeza hatua ya kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kueleza kuwa kanisa halikutoa msimamo wake juu ya muundo wa serikali unaotakiwa. Pia wameelezea hofu zao kuhusu uwepo wa dalili za baadhi ya vyama vya upinzani, kutaka kuvuruga mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya.

Pengo katika mkutano na waandishi wa habari juzi Dar es Salaam, alipinga waraka unaodaiwa kutolewa na Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kuhusu muundo wa serikali tatu na kusema sio wa Kanisa Katoliki nchini.

Wakizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, wajumbe hao wakiongozwa na Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (CCM), walidai kuwa wamefanikiwa kunasa mipango mbalimbali inayoratibiwa na baadhi ya watu ambao hawana nia njema na mchakato wa kupatikana kwa Katiba.

Alisema pamoja na kuandaa mikakati hiyo ambayo tayari mingine imeshaanza kukataliwa, ikiwemo waraka huo unaodaiwa kutolewa na Kanisa Katoliki wa kulazimisha uwepo wa serikali tatu.

"Katiba ni ajenda ya kitaifa lakini hivi sasa kumekuwa na maneno ya kila aina, hata wananchi kuaminishwa mambo yasiyo sahihi.

"Jana (juzi) mmesikia Kadinali Pengo ameukana ule waraka unaodaiwa kutolewa na Kanisa, nasi kama wajumbe kupitia CCM tunapongeza hatua hii, na sasa tumejua kila aina ya mbinu chafu za kukwamisha kupatikana kwa Katiba.

"Tunajua wazi katika kipindi hiki kuna hata baadhi ya nyaraka na vipeperushi, ikiwemo hata ujumbe kupitia baadhi ya mitandao ya jamii, ikiwa na lengo la kuaminisha jamii kuwa CCM ndiyo haitaki Katiba mpya, tunasema si kweli na Watanzania ni lazima wakatae kuburutwa na mawazo ya wanasiasa waliofilisika," alisema.

Zungu, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri la Muungano, alisema CCM haitasaliti uamuzi ulioamuliwa na wananchi isipokuwa haitakuwa tayari kuona Muungano ukivunjwa kwa tamaa ya madaraka.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalumu katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Haji Omar Kheir ambaye ni Mbunge wa Tumbatu, alikemea mipango inayoratibiwa na baadhi ya wanasiasa, ikiwemo kupandikiza chuki ili Muungano uvunjike.

"Tunajua wapo wanasiasa ambao wamekaa kuona bora Muungano uvunjike kwa tamaa ya kutaka madaraka, ili watawale, sisi wawakilishi tutasimama imara kupinga aina yoyote ya udhalimu huu.

"Nampongeza Pengo, kwani kwa imani yangu tutakwenda pamoja katika mchakato huu …zile taarifa za awali zilizodaiwa kuwa za Kanisa, nilikuwa najiuliza ni kweli taasisi kama hii ambayo inaheshimika na mamilioni ya waumini duniani inaweza kutoa tamko kama hili," alisema Kheir.

Naye Mjumbe wa Bunge hilo ambaye pia ni Mwakilishi wa Chwaka, Issa Haji Ussi, alisema CCM ni chama kinachoongozwa na misingi imara yenye kutetea matakwa ya wananchi.

"Kama mtu anataka kuvuruga amani, kwanza atambue kuwa atashughulikiwa yeye na Katiba mpya itapatikana ambayo italinda na kuimarisha Muungano wetu zaidi kwa miaka 50 ijayo," alisema Ussi.

Katika tamko la Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) inayoongozwa na Askofu Mkuu wa Tabora, Paulo Ruzoka, iliwekwa bayana kuwa muundo wa serikali mbili haukutatua matatizo ya msingi na badala yake ulilimbikiza kero zilizosababisha Zanzibar kujiundia Katiba yake mwaka 2010 bila kushauriana na Tanzania Bara.
pengo+px.jpg

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo akiwaonesha waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, nakala ya gazeti la Mwananchi lililoandika habari kuhusu msimamo wa Kanisa juu ya suala la serikali tatu.
Chanzo:Habarileo.
 
Kuna baadhi ya watu wanatumia njia zozote hata zile za kilaghai ili kupitisha ajenda zao. Wanashindwa kusimama wao wenyewe ili wahesabiwe kwa kutoa maoni yao kwa sababu pamoja na mambo mengine, wanasumbuliwa na inferiority complex. Hawajiamini kama kauli zao zinakubaliwa/zitakubaliwa na wanachi.

Huwezi kulitumia kanisa Katoliki kwa mambo ya kilaghai hasa ikichukuliwa kuwa kanisa ni kioo katika jamii kwenye maswala ya ubinadamu.

Kuelekea upatikanaji wa Katiba mpya, tutawasikia wengi wakija na matamko huku wakidai yametolewa na taasisi zinazo heshimika katika jamii.

Tunashukuru Baba Askofu kwa kutoa ufafanuzi mzuri kulingana na tamko la Tume ya Haki na Amani.
 
Mbona CCM mnahangaika sana? Ni nani aliwaambia kanisa katoliki linakwenda kinyume na matakwa ya wananchi?
 
Hao wakatoliki sasa ndio wanaonekana wa maana kwenye suala la katiba? Mnapowalipua kwa mabomu makanisani mbona huwa mnawadharau na kudai kuwa wamejilipua wenyewe?
 
Pengo alitoa maoni yake kama mtu binafsi na wala yeye sio msemaji wa kanisa la Tanzania. Mwenyekiti wa baraza la maaskofu katoliki Tanzania (TEC) ndiye msemaji wa kanisa Katoliki Tanzania. CCM msihalalishe hoja zenu zinazoenda kinyume na matakwa ya wananchi kwa mgongo wa kanisa!
 
Kuelekea upatikanaji wa Katiba mpya, tutawasikia wengi wakija na matamko huku wakidai yametolewa na taasisi zinazo heshimika katika jamii.Tunashukuru Baba Askofu kwa kutoa ufafanuzi mzuri kulingana na tamko la Tume ya Haki na Amani.
Hapo kwenye red umesema kweli kuhusu kile CCM inachokifanya.
 
Mwanadiwani tumekusikia ila wenye akili zao wanajua msimamo wa Wakatoliki katika hili ni upi. Hii kauli ya tume ya wakatoliki ni tofauti sana na kauli ya Pengo au ile aliyowahi kutoa Kilaini enzi zile kuwa JK ni chaguo la Mungu. Haya CCM wasiharibu mchakato huu kwa kisingizio cha Muungano, kwani tume ya Warioba imesema Muungano uvunjike? Sijui kwanini CCM mnahangaika kudhani eti kama kuna serikali tatu muungano utakufa. Ni kwamba tutakuwa na nchi ya Tanzania yenye serikali tatu basi mkihangaika na serikali mbili haya na Uamsho wameshatoka gerezani mtakutana nao Zanzibar.
 
Hao wakatoliki sasa ndio wanaonekana wa maana kwenye suala la katiba? Mnapowalipua kwa mabomu makanisani mbona huwa mnawadharau na kudai kuwa wamejilipua wenyewe?
Unataka kunionesha kuwa hiki ndiyo kipimo chako cha mwisho kifikra na kimtazamo?. You can do better than this!.

Anyway, the more you learn, the more you realize how little you know.
 
Viongozi wa dini mnalipeleka wapi taifa, mtu kama Pengo anapokubali kutumiwa na ccm kuliangamiza taifa, hii hatari, huu ni ushetani, naanza kupata shida na baadhi ya vingozi wa dini kama kina pengo, Mungu hawezi kuwaacha watu kama kina Pengo na ccm yake wakiliangamiza taifa, watu wamepigwa na kuuawa kwa mabomu kanisani kule Arusha, na kwenye kampeni za Chadema, leo kiongozi wa dini, askofu mkuu, anaposimama na kutumiwa na waharifu kuharibu mustakabari wa taifa ni hatari kubwa sana.
 
Mbona CCM mnahangaika sana? Ni nani aliwaambia kanisa katoliki linakwenda kinyume na matakwa ya wananchi?
CCM ndiyo kina nani?. Wana alama gani?.

Kanisa Katoliki ndiyo kina nani?. Lina alama gani

Wewe ndiyo nani?. Una alama gani tofauti na Kanisa Katoliki au CCM?.

Nina wasiwasi kama unaelewa hata unachoongea kwa njia ya maandishi!.
 
Unataka kunionesha kuwa hiki ndiyo kipimo chako cha mwisho kifikra na kimtazamo?. You can do better than this!.

Anyway, the more you learn, the more you realize how little you know.

Watu wa ajabu sana. Leo unasemabkanisa katoliki linaheshimika wakati wewe na timu yenu mnakesha hapa mitandaon kukashifu kanisa katoliki linaiburuza serikali kwa mfumo kristo? Nyie ni watu wa hovyo sana. Msitake kulitumia kanisa katoliki kama kiki ya kupata uhalali wa uharamia wenu
 
Pengo alitoa maoni yake kama mtu binafsi na wala yeye sio msemaji wa kanisa la Tanzania. Mwenyekiti wa baraza la maaskofu katoliki Tanzania (TEC) ndiye msemaji wa kanisa Katoliki Tanzania. CCM msihalalishe hoja zenu zinazoenda kinyume na matakwa ya wananchi kwa mgongo wa kanisa!
Wananchi ni kina nani na CCM ni kina nani?.

Maandishi yao yanaonyesha unataka kuogelea kwenye maji ya kisiasa wakati hufahamu hata basics za somo la uraia.
 
Mwenyekiti wa TEC ndio msemaji wa Kanisa Katoliki hapa Tanzania hivyo Pengo amekanusha kama askofu yeyote anavyoweza kufafanua lolote lakini Pengo amechemka kukanusha hilo kabla ya baraka za TEC ambao ndio wasimamizi wa kitengo cha haki na amani.

Kwanini kauli ya Pengo ionekane ndio msimamo wa Kanisa wakati hata Ruzoka ni askofu mwenye hadhi sawa na Pengo?
 
Kuna mazoea askofu wa jimbo kuu la Dar es salaam kuchukuliwa kama msemaji rasmi wa Kanisa.Waandishi wakitaka kupata maoni binafsi ya askofu waende kwa askofu lakini Kanisa linamsemaji wake rasmi.Pengo anachanganya waamini.
 
Wengi hawajui mfumo wa Kanisa Katoliki, wanadhani Pengo ndiye Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania. Pengo ni askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, ukuu wake unaishia pale, lakini TEC ndiyo chombo kikuu cha Kanisa Katoliki Tanzania. Pengo hayupo juu ya TEC.

Mwenyekiti wa TEC ndio msemaji wa Kanisa Katoliki hapa Tanzania hivyo Pengo amekanusha kama askofu yeyote anavyoweza kufafanua lolote lakini Pengo amechemka kukanusha hilo kabla ya baraka za TEC ambao ndio wasimamizi wa kitengo cha haki na amani.

Kwanini kauli ya Pengo ionekane ndio msimamo wa Kanisa wakati hata Ruzoka ni askofu mwenye hadhi sawa na Pengo?
 
Viongozi wa dini mnalipeleka wapi taifa, mtu kama Pengo anapokubali kutumiwa na ccm kuliangamiza taifa, hii hatari, huu ni ushetani, naanza kupata shida na baadhi ya vingozi wa dini kama kina pengo, Mungu hawezi kuwaacha watu kama kina Pengo na ccm yake wakiliangamiza taifa, watu wamepigwa na kuuawa kwa mabomu kanisani kule Arusha, na kwenye kampeni za Chadema, leo kiongozi wa dini, askofu mkuu, anaposimama na kutumiwa na waharifu kuharibu mustakabari wa taifa ni hatari kubwa sana.
Wewe ndiyo unalipeleka taifa kubaya kwa sababu maandishi yako yanaonyesha hujitambui na kwa maana hii, hufahamu hata unachokiandika achilia mbali kuelewa hoja anayoisema Baba Askofu.
 
Watu wa ajabu sana. Leo unasemabkanisa katoliki linaheshimika wakati wewe na timu yenu mnakesha hapa mitandaon kukashifu kanisa katoliki linaiburuza serikali kwa mfumo kristo? Nyie ni watu wa hovyo sana. Msitake kulitumia kanisa katoliki kama kiki ya kupata uhalali wa uharamia wenu
Beware of false knowledge; it is more dangerous than ignorance-George Bernard Shaw

Unapoleta serious accusation kama hizi ni lazima uweke bandiko hapa ambalo linaonyesha nikikashifu Kanisa Katoliki.

Unafahamu imani yangu ya dini au ndiyo yale yale ya false knowledge.

Ni afadhari kufahamu kuwa hufahamu ili upate msukumo wa kujifunza zaidi kuliko kudhani unafahamu wakati hufahamu na matokeo yake ni kuzidi kuzama kwenye ujinga na viroja kama ulivyovileta hapa.
 
Mie nafikiri watu hamjamuelewa Cardinal Pengo, anasema serikali mbili kwa maana kwamba Zanzibar walishavunja katiba na kuwa na serikali yao sasa; Bendera, wimbo wao wa taifa n.k. Au hadi tupigane vita ndio tuwaruhusu wajitenge? Watanganyika wawe na ya kwao. Ndio maana ya serikali mbili.
Sio serikali mbili tena kwa maana ya Bara na Muungano. kwani hiyo ilishakufa siku nyingi. kilichobaki ni kiini macho.
 
Kuna mazoea askofu wa jimbo kuu la Dar es salaam kuchukuliwa kama msemaji rasmi wa Kanisa.Waandishi wakitaka kupata maoni binafsi ya askofu waende kwa askofu lakini Kanisa linamsemaji wake rasmi.Pengo anachanganya waamini.
Haya ni mawazo yako na haikatazwi kukaa nayo lakini usilijengee hoja kanisa na hasa Baba Askofu kuwa huwa anajichukulia majukumu ya kikanisa ambayo siyo yake.

Baba Askofu anafahamu mipaka ya kazi yake vizuri lakini kwa sababu hoja aliyoleta inakinzana na mtazamo wako, ndiyo maana unaanza kutafuta upenyo ndani ya mgawanyo wa madaraka ya kanisa ili kuiua hoja yake.

Ukweli wa hoja yake utaendelea kusimama kama ilivyo kazi yake iliyomfikisha katika nafasi aliyonayo kwa sasa. Tatizo ni kwamba, Baba Askofu, Mwadhamu Polycarp Pengo hana unafiki ambayo wengi wangetemea awe nao kama walivyo wao.
 
Kuna baadhi ya watu wanatumia njia zozote hata zile za kilaghai ili kupitisha ajenda zao. Wanashindwa kusimama wao wenyewe ili wahesabiwe kwa kutoa maoni yao kwa sababu pamoja na mambo mengine, wanasumbuliwa na inferiority complex. Hawajiamini kama kauli zao zinakubaliwa/zitakubaliwa na wanachi.

Huwezi kulitumia kanisa Katoliki kwa mambo ya kilaghai hasa ikichukuliwa kuwa kanisa ni kioo katika jamii kwenye maswala ya ubinadamu.

Kuelekea upatikanaji wa Katiba mpya, tutawasikia wengi wakija na matamko huku wakidai yametolewa na taasisi zinazo heshimika katika jamii.

Tunashukuru Baba Askofu kwa kutoa ufafanuzi mzuri kulingana na tamko la Tume ya Haki na Amani.

Kwa hiyo Polycarp Pengo akuruhusu ushoga uta-validate kwa kuwa cardinal amesema hivyo?
Can't you see Pengo au Pope ni binadamu wa kawaida kama wewe na mimi?
 
Back
Top Bottom