Wabunge, Wawakilishi na wajumbe wa Bunge la Katiba wapongeza msimamo wa Kanisa Katoliki.

Wabunge, Wawakilishi na wajumbe wa Bunge la Katiba wapongeza msimamo wa Kanisa Katoliki.

Kwa hiyo Polycarp Pengo akuruhusu ushoga uta-validate kwa kuwa cardinal amesema hivyo?
Una maana gani katika hii hoja yako?. Hoja yako niya kitoto!.
Jenga hoja kwa kutumia mifano ya halisi na siyo kwa jinsi unavyofikiria. Kwa akili yako unafikiria Baba Askofu ataruhusu ushoga au kwa maana hyingine, unadhani Baba Askofu atatenda kinyume na imani inayomfanya awe Baba Askofu na aendelee kuwa Baba Askofu.
Can't you see Pengo au Pope ni binadamu wa kawaida kama wewe na mimi?
Pope au Mwadhamu Polycarp Pengo siyo binadamu wa kawaida katika imani ya kanisa Katoliki kama unavyotaka kutuaminisha na ndiyo maana hata jina lake limebeba uzito kiimani katika Kanisa Katoliki.

Kama wewe siyo Mkatoliki, basi huwezi kuelewa mantiki ya andiko langu!.
 
"Vya Caesar mpeni caesar na vya Mungu mpeni Mungu" otherwise mta2peleka shimoni.
 
CCM kimekuwa ni chama cha upinzani na ndicho kinachoivuruga rasimu ya katiba kwa kupinga maoni ya wananchi ili ipatikane katiba ya ki CCM CCM wakati wananchi wanahitaji katiba yenye sura ya kitaifa.
 
CCM CCM mbona mnashikwa na HOMA? Pengo amesema mapendekezo yake kuhusu Serikali mbili ni mtazamo wake na sio msimamo wa Kanisa. Nijuavyo Askofu Ngalalekumtwa wa jimbo la Iringa ndiye raisi wa TEC ambaye ndiye msemaji mkuu wa Kanisa sio Pengo. Serikali Tatu hazikwepeki, hilo CCT na TEC wanajua hivyo. mawazo na tofauti ya mitizamo lazima iwepo lakini msingi wa hoja utabaki pale pale.
 
Kuna baadhi ya watu wanatumia njia zozote hata zile za kilaghai ili kupitisha ajenda zao. Wanashindwa kusimama wao wenyewe ili wahesabiwe kwa kutoa maoni yao kwa sababu pamoja na mambo mengine, wanasumbuliwa na inferiority complex. Hawajiamini kama kauli zao zinakubaliwa/zitakubaliwa na wanachi.

Huwezi kulitumia kanisa Katoliki kwa mambo ya kilaghai hasa ikichukuliwa kuwa kanisa ni kioo katika jamii kwenye maswala ya ubinadamu.

Kuelekea upatikanaji wa Katiba mpya, tutawasikia wengi wakija na matamko huku wakidai yametolewa na taasisi zinazo heshimika katika jamii.

Tunashukuru Baba Askofu kwa kutoa ufafanuzi mzuri kulingana na tamko la Tume ya Haki na Amani.

Mkuu vipimo vinaonyesha kuwa Mwana Diwani anasumbuliwa na inferiority complex. Na hii nikutokana na yeye kutojua mawazo ya mtu binafsi na mawazo ya Jumuiya ni yapi. Hivyo Mwanadiwani anapaswa kuzingatia yafuatayo. Msemaji wa kanisa Katoliki Tanzania ni Mwenyekiti wa baraza la maaskofu (TEC)
 
Mkuu, huyo mwendawazimu anajua vizuri sana ila anajitoa tu ufahamu simply kwa kuwa amekutana na ka-point kwenye kauli ya Pengo ambako kako in favour of CCM. Hayo mengine yote hayaoni isipokuwa "maoni binafsi" ya Pengo ndiyo ya muhimu kwake; giliba kama kawaida ya magamba.

Najarajibu kuwaza kama Pengo "angeteleza" akasema kwa maoni yake, kwa mfano, haoni ni haki Mahakama ya Kadhi kuwemo ndani ya Katiba Mpya. Usitegemee MwanaDiwani na mateja wenzake pale Lumumba wangeongea alivyoongea in favour of Pengo; sana sana ungesikia Chadema yatoa kauli kupitia wakatoliki kupinga mahakama ya kadhi. Yaani haya majitu nin manafiki hakuna mfano.
 
Last edited by a moderator:
Mwanadiwani tumekusikia ila wenye akili zao wanajua msimamo wa Wakatoliki katika hili ni upi. Hii kauli ya tume ya wakatoliki ni tofauti sana na kauli ya Pengo au ile aliyowahi kutoa Kilaini enzi zile kuwa JK ni chaguo la Mungu. Haya CCM wasiharibu mchakato huu kwa kisingizio cha Muungano, kwani tume ya Warioba imesema Muungano uvunjike? Sijui kwanini CCM mnahangaika kudhani eti kama kuna serikali tatu muungano utakufa. Ni kwamba tutakuwa na nchi ya Tanzania yenye serikali tatu basi mkihangaika na serikali mbili haya na Uamsho wameshatoka gerezani mtakutana nao Zanzibar.

Muungano siyo pumzi ya watanzania hata ukivunjika tutaendelea kupumua na kuishi, CCM wasififishe matakwa ya watanzania kwa kigezo cha muungano. Watanzania hawajasema hawataki muungano ila wanataka uboreshwe.
 
CCM Pengo siyo muamuzi wa wakatoliki Tanzania, sisi waumini tunataka serikali Tatu, kama yeye hataki ni juu yake.
 
The game is over, serikali 3 ni ndoto za mchana.
 
Tido mhando,asipokuwa makini,waandishi na wahariri wake watashusha hadhi ya gazeti la mwananchi,sii mara moja gazeti hili limeripoti taarifa za uwongo,liliwahi kumnukuu uwongo askofu kilaini,kesho yake akajitokeza hadharani kwamba hakuwahi pigiwa na mwandishi kumuuliza hayo walodai maoni yake,mifano ya gazeti kusutwa ni mingi,namuomba tido afikirie tena na tena.
 
Wakuu Msaada, mwenye taarifa Kikao cha bunge la katiba leo ni saa ngapi?
 
Kuna mazoea askofu wa jimbo kuu la Dar es salaam kuchukuliwa kama msemaji rasmi wa Kanisa.Waandishi wakitaka kupata maoni binafsi ya askofu waende kwa askofu lakini Kanisa linamsemaji wake rasmi.Pengo anachanganya waamini.
Mkuu hili ndo janga la taaluma ya habari nchini. Tamko limetoka TEC waandishi wanataka ufafanuzi toka kwa Pengo ambaye kesha jipambanua ni muumini wa serikali mbili kinyume na matakwa ya wengi. Kwa hili pana walakini katika uongozi wake hapo jimboni, nadhani ni wakati wa Vatican kumtafutia nafasi huko.
 
Muungano siyo pumzi ya watanzania hata ukivunjika tutaendelea kupumua na kuishi, CCM wasififishe matakwa ya watanzania kwa kigezo cha muungano. Watanzania hawajasema hawataki muungano ila wanataka uboreshwe.
Hili la uboreshaji wa muungano hawa CCM masilahi hawalielewi. Nahisi Pengo anatetea uhai wake maana aliisha tuambia anatishiwa.
 
Mfumo kristo ndio huo unaanza kujichanganya wenyewe. Wazidi tu kumpa maelekezo yao Prof Costa mahalu awakilisha matakwa yao vizuri.
 
Hao wakatoliki sasa ndio wanaonekana wa maana kwenye suala la katiba? Mnapowalipua kwa mabomu makanisani mbona huwa mnawadharau na kudai kuwa wamejilipua wenyewe?

Si hilo tu Honolulu, kumbuka hawa wakatoriki walipotoa WARAKA wao kuelekea uchaguzi mkuu 2010 jinsi CCM walivyowananga. Pia hawa WAKATORIKI wameshutumia sana na CCM kwamba 2010 walimsaidia mgombea fulani kwa kumpigia kampeini makanisani. Sijui leo CCM wamepata wapi UJASIRI wa kuwasifia Wakatoriki! Kweli unafiki ni kitu kibaya.
 
Una maana gani katika hii hoja yako?. Hoja yako niya kitoto!.
Jenga hoja kwa kutumia mifano ya halisi na siyo kwa jinsi unavyofikiria. Kwa akili yako unafikiria Baba Askofu ataruhusu ushoga au kwa maana hyingine, unadhani Baba Askofu atatenda kinyume na imani inayomfanya awe Baba Askofu na aendelee kuwa Baba Askofu.

Pope au Mwadhamu Polycarp Pengo siyo binadamu wa kawaida katika imani ya kanisa Katoliki kama unavyotaka kutuaminisha na ndiyo maana hata jina lake limebeba uzito kiimani katika Kanisa Katoliki.

Kama wewe siyo Mkatoliki, basi huwezi kuelewa mantiki ya andiko langu!.

Pope na cardinal Pengo ni binadamu wa kawaida kama wewe na mimi
 
Back
Top Bottom