Wabunge wengi hawakubaliani na utawala uliopo bali wanauheshimu?

Wabunge wengi hawakubaliani na utawala uliopo bali wanauheshimu?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
761
Reaction score
6,985
Kila Mbunge anayesimama bungeni anakosoa utaratibu unaotumiwa na awamu ya tano kuendesha Mambo yake. Kwa mfano;

Sospeter Muhongo katika vipaumbele vyake vitano anavyopendekeza hakuna hata kimoja ambacho amekieleza kwa mrengo wa kukubaliana na vipaombele vya serikali iliyopo. Ametaja kilimo, nishati ila akasema isiwe ya aina moja bali tupate nishati kutoka vyanzo tofauti, ametaja gas ambayo kila mmoja anajua awamu ya tano haikubaliani na kilichofanyika Mtwara nk.

Nape Nnauye amepingana na dhana ya Task force kutumika kukusanya Kodi akitaka suala la Kodi lirudi TRA, hoja hii iliibuliwa toka mwaka 2016 lakini hakuna mwana CCM aliyeunga mkono wakati huo.

Msukuma anazungumzia kuwekeza kwa watu, hii hoja ni kongwe na kwamba matrilion ya fedha za umma yameelekezwa kusiko zalisha. Lakini msukuma huyuhuyu ndiye aliyeshadadia uanzishwaji wa miradi hii mikubwa inayoonekana leo haina tija.

Wabunge wetu mnatuchanganya, Leo yes kesho no with no reason. Acheni KULALAMIKA, mnavuna mlichopanda na msitegemee awamu hii itaisha aje mwingine. Chungeni ndimi zenu shaurini yaliyyo na tija kwa Taifa...msisome upepo
 
Hili ndio bunge sio kutukana hapa naona bunge na rais kawaambia wawabane mawaziri kwelikwel.
 
Kama wanaheshimu na hawakubaliani Basi,wako vizuri...kwa sababu wameweka mbele uzalendo,na kutupilia mbali matamanio yao binafsi.
 
Kukosoa si tiketi ya kutokukubaliana na utawala, lakini pia kusifia si mwamvuri wa kukubaliana na utawala bali wanaokubaliana na utawala ni wote wenye hoja za kulijenga taifa. Wasiokubaliana na utawala ni wale tu wanaodhani Wazungu ndio mwarobaini wa matatizo Yao kwa mfano wale walioenda kula ubwabwa wa bure ulaya wakati sisi tunajenga taifa. Njaa na uvivu umewapeleka "ASYLUM "
 
Kunambi anataka kumtoa Lukuvi akaipime Tanzania nzima kwakutumia vijana wake walio ipima Dodoma kijana ni hatare sana alimngoa Rc wake jina limenitoka Mzee Lukuvi ukicheka na Nyani utavuna mabua
 
Hili ndio bunge sio kutukana hapa naona bunge na rais kawaambia wawabane mawaziri kwelikweli
Kwa hiyo rais anawatuma wabunge na si wananchi kuwakilishwa na wabunge wa majimbo yao.

Utawala kimeo sana huu.
 
Tuliopiga kula tunajua tulichofanya wewe vilaza wako wamekimbia nchi kazi ni kwako
Kama ni hivi hakuna utashi katika uongozi/utaw ala wa JPM, ndio maana alichagua wabunge wake kutoka mifukoni mwake.
 
Bunge Kibogoyo! Bunge lililojaa wanafiki, Vilaza na wachumia tumbo. Kimsingi halina faida wala tija yoyote ile kwa Watanzania.
 
Pamoja na yote, ndugu yangu watu wanachangia kwa kuvizia aseee hujui..?

Wanajua mtawala aliyepo siyo rafiki, so kila mtu ana hofu na hatima ya maisha yake.
 
Back
Top Bottom