Mchokozi wa mambo
JF-Expert Member
- Mar 27, 2014
- 201
- 159
Nimekuwa nafuatilia mijadala na vikao mbalimbali vya bunge letu hata wawapo majimboni hawatetei nchi wala wananchi ambao kimsingi wanawawakilisha. Muda wote wanamsifia mama Samia. Wote ni chawa ukiwatoa wawili tu Mhe. Luhaga Mpina na Sanga wa Makete angalau unawasikia wanaongea nini na wanafanya kazi za kibunge. Inaumiza sana kuona mfano tu wa hivi karibuni kuhusu mjadala wa Bandari yetu. Hakuna walichong'amua zaidi walikuwa wanamsifia Samia na kumshambulia Mbowe. Suala la maslahi kwa taifa kwao sio kipaumbe bali kipaumbele kwao ni matumbo yao