Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Nchi hii, kuna watu wengi wenye elimu nzuri na akili pia, LAKINI unafiki wao na uchawa vimewafanya wapoteze weledi na akili ya reasoning na argument, kiasi cha kuwafanya waonekane kama ni watu wasio na weledi wala uelewa.
Tambueni kuwa Spika Tulia ni mwanasheria, tena mwenye shahada tatu kwenye sheria, lakini ananyoyatenda kwa sasa dhidi ya Mbunge Mpina, hata mtu ambaye ana certificate ya sheria, anayejua na kuheshimu katiba, hawezi kuyafanya.
Tulia hajua kuwa haki ya kwanza ya kila mwananchi, ni haki yake ya uraia. Na haki hiyo haipotei kwa mtu mtu huyo ni mbunge, diwani au Waziri.
Mpina aliitisha vyombo vya habari, kama raia wa Tanzania na kama mbunge. Tulia ni kiranja wa wabunge wawapo ndani ya vikao vya Bunge. Yeye siyo mkuu wa wabunge wawapo nje ya vikao vya Bunge. Mpina, kama mbunge, anapoenda kwenye vikao vya Bunge, anawawakilisha wananchi wake. Na kama kumetokea mtafaruku wowote huko kwenye vikao vya Bunge, ana haki ya kuwajulisha wapiga kura wake juu ya kilichojiri huko Bungeni, na ana haki pia kuwajulisha wananchi wake anapeleka majibu gani Bungeni kuhusiana na alichoelekezwa na kiranja wa vikao vya Bunge.
Kwa mujibu wa katiba, Mpina kama raia wa Tanzania, kama mbunge mwakilishi wa wananchi, hakiuki sheria yoyote katika kufanya kikao chochote na mtu yeyote akiwa nje ya Bunge. Tulia hana mamlaka ya kumuamlia Mbunge Mpina au mtu mwingine yeyote, aukutane na nani au aseme nini akiwa nje ya vikao vya Bunge.
Hivyo, Tulia kuelekeza kuwa Mpina ahojiwe na kamati ya kanuni na maadili ya Bunge eti kwa nini alifanya kikao na wanahabari wakati hakuwa chini ya mamlaka ya spika, ni kuishiwa weledi na reasoning hata ile ya kawaida. Kama Mpina alikiuka sheria yoyote ya nchi kwa kufanya kikao na wanahabari akiwa nje ya Bunge, wa kumwajibisha siyo Spika Tulia. Nje ya Bunge kuna vyombo vya kusimamia sheria, na vyombo hivyo, siyo Spika wa Bunge.
Spika Tulia amka, uondoke kwenye usingizi wa mahaba ya mambo ambayo hayapo kisheria. Usiwe mtumwa wa mahaba bali mtumwa wa weledi, ndivyo watu wenye hekima wanavyokuwa.
Wabunge nanyi, pamoja na kwamba wengi wenu ni zao la uovu wa uchaguzi wa 2020, kama mna weledi japo kidogo, mwondoeni Tulia kwenye hiyo nafasi kwa kukiaibisha kiti cha spika, kwa kutenda mambo yaliyo kinyume na katiba ya nchi. Katiba ya nchi ipo juu ya kanuni na maadili ya Bunge. Heshimuni katiba kwanza, kabla ya chochote.