Wabunge wenye Hekima, waazimie kumfukuza Spika Tulia

Spika Tulia yuko sahihi

Kuumwaga ushahidi nyeti wa kiserikali hadharani ni kuhatarisha Usalama
TULIA ana akili nyingi sana!!

Anajua uwezo wa Mpina katika kuandaa na kuwasilisha ushahidi. Si mara Moja au mara mbili Mpina alitakiwa kufanya hivyo na akafanya Kwa viwango vya juu sana. Supika Tulia anaujua uwezo wa Mpina na Sina shaka kwamba ni Tulia huyu huyu ndiye aliyetamani Mpina amwage mtama penye kiku wengi!!

TULIA ana akili kuliko wengine, bila kumpeleka Mpina kwenye Kamati ya Maadili angeshukiwa mbaya kutoka alikoshitakiwa Ndugai!!

Wenye akili tumekuelewa Supika Tulia; na ujumbe umetufikia bila mawaa
 
Ohooo 😳
 
Umeongea Kitu kikubwa Sana 😄
 
Tunaongelea maslahi ya Taifa sio chama. Pia hoja ilikuwa ya Mpina kuwasilisha Ushahidi, akaona auweke wazi Kwa umma ili hata Tulia akiuficha apatikane.
Mkuu viongozi wetu wengi wao wanaongozwa na maslahi binafsi siyo ya umma, ndomana kauli na matendo yao yanategemea mkuu wa kaya amekaaje.
 
Ukisoma comments za watu wote humu, bila shaka unaelewa wazi kuwa huyu Bigstone ndiye punguani wa pekee.

We ignore such mind crippled creatures
Wagonjwa wa akili kama huyu ni wa kuwapuuza.
Watu wa aina yenu ndiyo mmeishusha hadhi JF.
 
Hii ni tweet ya Ruto.

Na hapo kajibiwa na jaji mkuu mstaafu wa Kenya Willy Mutunga.

Rais Ruto anaulizwa ni kwa mamlaka gani ameyatumia kutuma polisi kwenda kuzuia jambo ambalo ni haki ya kikatiba "maandamo/mkusanyiko ilhali aliapa kuilinda katiba.

Maandamano ya amani yanaruhusiwa kikatiba katika kifungu cha 37 kwenye katiba ya Kenya ya mwaka 2010.

Kwa Tanzania nani leo hii kama mkuu wa ile mihimili aidha aliyepo madarakani au mstaafu atajitokeza kumkosoa Samia kwa namna anavyoendesha nchi

Nchi inaibiwa imebaki kama chandarua chenye matundu lukuki huku Samia kila siku yupo angani tu.?

Leo hii mkuu wa mhimili kama Rango japo hakuchaguliwa bali aliingia kwa nguvu ya mtutu anageuka kuwa chawa wa rais.
 
Wabunge wenye hekima na akili walishatoweka tangu April 2020 sasa hivi kuna machizi tu mara wapige sarakasi mezani mara wakate mauno yaani yule mwovu alituweza kweli watanzania.
 
Spika Tulia yuko sahihi

Kuumwaga ushahidi nyeti wa kiserikali hadharani ni kuhatarisha Usalama
Kama alihatarisha usalama si kuna vyombo vya usalama. Kwa nini hawajamshughulikia badala yake anapelekwa kwenye Kamati ya maadili bungeni. Hii nadhani si sawa
 
Ulitaka yale aliyosema Mhe. Mpina mbele ya Wanahabari yawe SIRI KUBWA kwa Bunge. La hasha. Kumbe mengi yamefichwa na Bunge haya ya Mpina ni kama tone la maji kwenye bahari.
 
Tutafika tu huko 🙄
Tutakuwa na Strong Institution’s 🤠
 
Spika Tulia yuko sahihi

Kuumwaga ushahidi nyeti wa kiserikali hadharani ni kuhatarisha Usalama
Lakini halipo chini ya mamlaka ya spika Bali mamlaka nyinginezo za usalama. Spika amelidandia lisilompeleka aendako!
 
tukimuuliza wakili mwabukusi kule mbeya atakujibu tulia hafai hata kuwa mama wa familia...kuna wakati anavaa vipensi anacheza hadharani...sasa bunge mmemkabidhi si balaa hilo 😎
 
Tanzania Ina mataahira wengi sana! Wewe unajielewa, waambie ukweli Hawa mapimbi hawaelewi kabisa! Kama yule mpuuzi alisema tuende Burundi! Kenya wameandamana na tozo 14 zimeondolewa!
 
Spika Tulia yuko sahihi

Kuumwaga ushahidi nyeti wa kiserikali hadharani ni kuhatarisha Usalama
Hao Jeshi la Polisi lililomwaga ushahidi nyeti Sana Tena ushahidi wa Nyaraka za Siri za Serikali hadharani kuhusu suala la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Rajab Nawanda wamechukuliwa hatua gani za kisheria????
Tena hao Polisi wamefanya kosa kubwa zaidi la UHAINI kwa kuanika hadharani hizo Nyaraka za Siri za Serikali, kwa Nini Kuna double standards??
Waanze kwanza kuadhibiwa Jeshi la Polisi Kisha afuatie huyo Luhaga Mpina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…