Wabunge wenye Hekima, waazimie kumfukuza Spika Tulia

Naunga mkono hoja. Huyu supika ni kaputi kutokana na uchawa. Weledi umemwishia kabisa. Nilisikitika sana wakati alipotishia watu eti yeye ndio yuko kwenye nafasi kwa hiyo aachwe kuamua bila kusemwa au kupingwa. Hakika inashngaza. Sitasahau hila alizotumia hadi kupitisha bungeni ule mswaada wa kukabidhi bandari za nchi yetu zote kwa dubai na kutetea hadi kuwaita wazalendo waliyopinga kwa nguvu zote wapumbavu. Mkataba wenyewe ni sawa na ile nyerere alisema kubadilishana gololi kwa dhahabu. Kigogo mmoja mzalendo mungu ambariki akasema mkataba wenyewe haufai hata kulumangia ugali.
 
Ule mkataba wa kishenzi wa bandari, kuna siku majina ya wahusika wakuu wote yatawekwa wazi na kutangazwa kama maadui wa Taifa waliotumia nafasi zao kuliangamiza Taifa. Katika orodha hiyo, Tulia hatakosekana.
 
Hata kama ningekuwa sikubaliani na hoja yako, lakini uandishi ulioonyooka namna hii unafurahisha na kuleta heshima ndani ya JF.

Huyu binti, tokea mwanzo, hata akiwa naibu wa Ndugai, nilimwona kuwa mtu wa matatizo. Wakati ule alipoteuliwa kabla ya kuukwa Naibu Spika na kuonyesha uhayawani wake, nilijuwa kuwa uteuzi wake ulifuata tabia zilezile alizokuwa akizipenda Magufuli; na hili lilikuja kujidhihirisha alipoukwaa unaibu spika wenyewe.

Nchi hii tunayo bahati mbaya sana, wasomi vichaa ndio mara nyingi wanajitokeza kuwa mbele, huku wasomi wenye utulivu wa akili wakibaki kuwa kama matrela tu wa kuvutwa na vichaa hawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…