BRELA
Govt Institution
- Dec 14, 2023
- 119
- 89
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umewahimiza wabunifu nchini kusajili kazi zao ili kuzilinda kisheria, Wakala imeeleza kuwa usajili huo utawasaidia wabunifu kuzipa thamani kazi zao na kufungua fursa mpya za kibiashara na kiuchumi.
Hayo yamebainishwa na Msajili Msaidizi Mwandamizi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi. Neema Kitala, Agosti 18, 2026, wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, mkoani Tanga.
Amesema ubunifu uliosajiliwa unaweza kuwa mali yenye thamani ambayo mbunifu anaweza kuitumia kama fursa ya kibiashara kupitia mauzo, makubaliano ya matumizi au ushirikiano na watu na taasisi nyingine.
“Ubunifu uliosajiliwa unakuwa mali yenye thamani ambayo mbunifu anaweza kuiuza, kuingia makubaliano na mtu au taasisi nyingine ya kuitumia au kuendeleza teknolojia hiyo na kupata manufaa ya kifedha,” alisema Bi. Kitala.
Aidha, Afisa Usajili kutoka BRELA, Bw. Benedickson Willson, amesema ubunifu unaolenga kutatua changamoto za jamii unaweza kuwa na thamani kubwa endapo utalindwa na kutumiwa ipasavyo.
“Usajili wa ubunifu, nembo, michoro, bidhaa mpya na teknolojia mbalimbali unampa mbunifu haki ya kipekee ya kutumia kazi yake na kumkinga dhidi ya watu wanaoweza kuitumia bila ruhusa,” alisema Bw. Willson.
BRELA imewahimiza wabunifu kutembelea banda la Wakala katika maadhimisho hayo ili kupata elimu kuhusu huduma zinazotolewa, hususan usajili na ulinzi wa haki za miliki bunifu, kwa lengo la kuhakikisha mawazo yao hayabaki kuwa mawazo pekee, bali yanageuka kuwa mali yenye thamani na fursa ya kiuchumi.