Wacha nimpe darasa kidogo Mzee Jakaya Kikwete

Na Mwl John Pambalu

Nimeshangazwa sana na kauli ya mzee Kikwete aliyoitoa jana huko mkoani Mara siku moja baada ya tamko la Baraza la maaskofu Katoliki katika kile alichodai kuwa si sawa kuchanganya dini na siasa.

Kikwete ambaye marehemu Askofu Getrude Lwakatare alikuwa mbunge kupitia chama chake CCM na hakuwahi kuitoa kauli kama hiyo anayoitoa sasa. Kikwete ambaye Askofu Gwajima anayezunguka kuhubiri nchi nzima huku akitumia madhabahu kumnadi Rais Samia, wabunge na madiwani kwenye madhabahu na Kikwete alichagua kunyamaza. Kikwete ambaye Sheikh Mkuu wa Dar es laam Sheikh Walid Alhad aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Malezi wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Dar es laam, Kikwete alichagua kukaa kimya. Nini kinamtoa pangoni sasa?

Kwanza, upo uwezekano kuwa yumo kwenye scandal ya bandari kupewa waarabu so anatetea mkate wake wa kila siku.

Pili, anaona CCM chama chake kinaenda kuanguka kwa kukosa ushawishi kiasi kwamba sasa wanaogopa nguvu ya maaskofu katika ku speedup anguko la CCM kutokana na uovu wao.

Tatu: Unafiki.

Sasa wacha nimpe Darasa.

Mzee JK akimuona askofu ajue huyo askofu ameshirikishwa Ukuhani, Unabii na Ufalme wa Kristu. Leo nitazungumzia unabii tu na nitatolea mifano ya manabii wawili, Nabii Samweli na Nabii Nathani.

Zamani Mungu aliwatumia manabii kuwapaka watu mafuta ili wawe wafalme rejea 1 Samweli 9:17 "Huyu ndiye mtu niliyekwambia habari zake! Yeye ndiye atakayewatawala watu wangu". Hapa Nabii samweli anaambiwa amsimike mfalme Sauli kuwa nabii wa Israeli. Hii hata nchini kwetu huwa tunafanya, wakati wa kumuapisha Rais viongozi wa dini wanaalikwa ili washuhudie ama kushiriki kumsimika Rais mteule.

Hata katika kumkataa mfalme Mungu hutumia manabii Rajea 1 Samweli 16:1-7 "BWANA akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israel?". Samweli aliyetumika kumsimka Sauli kuwa nabii, Samweli yuleyule anatumiwa tena kuambiwa kuwa Mungu amemkataa Sauli.

Nafikiri unaweza ona namna dini na siasa zilivyokuwa zikihusika tangu Mwanzo katika kuwaweka na kuwaondoa wafalme.

Wakati fulani mfalme Daud alimchungulia mke wa mwanajeshi wake akioga yule mwanajeshi alikuwa akiitwa Huria. Akamtamani akalala na yule mwanamke, mwanamke akapata mimba, Daud akaagiza mumewe arejeshwe kutoka jeshini ili amlishe, amnyweshe na amuache akalale na mkewe ili ionekane ile mimba ni yake (Deception)

Mwanajeshi akarudi kweli akala na kunywa ila kwa kuwa alikuwa akijua miiko ukiwa vitani huruhusiwi kulala na mkeo hakwenda kulala na mkewe. Mfalme akakasirika akaagiza apelekwe kwenye mapambano makali vitani ili apigwe afe. Kweli akauawa vitani, mfalme Daud akamchukua mke wa yule jamaa.

Mungu akakasirika akamtuma nabii Nathani aende kumuonya mfalme Daud Rejea 2 Samweli 12:1-25 Mfalme Daudi akalia akatubu akisema, “Nimetenda dhambi dhidi ya Mwenyezi-Mungu.” Mungu akamsamehe akaendelea kutawala Israel.

Nataka kusema nini?

1. Kama Nabii Nathani (wa dini) alimuonya mfalme Daudi (wa siasa) dhambi iko wapi maaskofu kumkemea Rais Samia?

2. Kama Mfalme Daudi alijua makosa yake akanyenyekea na kutubu na kuacha njia yake mbaya, kwa nini Rais Samia asitazame nyuma na kuachana na mkataba ovu wa Bandari. Ili aendelee kutawala kwa amani bila pressure kutoka kwa umma wa anaowaongoza?

Nafikiri Rais bado anayo nafasi, asimsikilize Kikwete bali aangalie wapi kajikwaa, apige chini mkataba wa bandari, asimame tena asonge mbele akiwa na uhakika kuwa kama kuna mahali alifanya vibaya kwa hila, rushwa ama upendeleo Mwenyezi Mungu ni mwingi wa Rehema na Neema atamsamehe na kumuimarisha tena maana hatujakamilika huo ndiyo ubinadamu wetu.

La! akishupaza shingo maneno haya yatamuhusu. Arejee Daniel 5: 24-28 Ndipo kile kitanga cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya yameandikwa. Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI. Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha. TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka. PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.

Wasalaam
John Pambalu
Pretoria - Afrika Kusuni
21.08.2023
Injili safi na mardadi toka Kwa mwalimu. Asante sana Pambalu
 
Kama Taifa tunayo bahati mbaya kuwa na viongozi wa kitaifa wanafiki na wameliumiza Taifa kwa kuwaambukiza wafuasu wao, hatuna kiongozi alienyooka anymore ambaye anaweza kuusema ukweli hata kama unakata maslahi yake nchi imekuwa ya kiunafiki ya level hatari kutokana na unafiki wa hawa watu wetu

Halianguliwi papai mnazini.

Viongozi wetu wanatokana na sisi wananchi. Misingi yetu, vipaumbele vyetu, matakwa yetu na matamanio yetu yanaumba aina ya viongozi tulionao.

Tukiukubali ukweli huu mchungu, tutavuka hatua kubwa sana. Sana!
 
Mkuu, kwani JK ana maajabu gani, kuwa kiongozi bongo hakuna uhusiano wowote na kuwa na akili!.
Siunaona hata std 7 wamo mjengoni.
🤣🤣Jk alifeli chuo
Yani walimpa tu gentomen degree ya 2.0,au wadau waiweke hadharan?afu wauwae?🤣🤣hakuna hiyo
Jua tu,yeye, mwanae rizmoko na mkewe mwalimu wa upe kilaza🤣🤣
Pale aongee Dokta salama tu🙏👌🤣
 
Pambalu viatu vinakupwaya!!

Vijana CDM hawana hamasa na Ari kama zamani, enzi ya Mnyika na Heche BAVICHA ilifana.

Mrema anazuiwa interview star tv upo upo tu Badala ya kuruka na pena!!!

Changamka!!!

Please don't take it personal🙏🙏
 
JK kasahau kuwa chama chake kiliwaita viongozi wa dini kuwashirikisha suala la mkataba wa DP World? Mzee kajichanganya zaidi kutumia madhabahu kukemea dini kuchanganya na siasa yaani anakemea kitendo anachofanya yeye mwenyewe. Mbaya zaidi kutumia mimbari ya Wasabato kuwakabili Wakatoliki ilhali inajulikana wazi kuwa Wasabato hawawivi na Wakatoliki.
Uko sahihi kabisa
 
Attachments

  • FB_IMG_1688651214549.jpg
    FB_IMG_1688651214549.jpg
    57.8 KB · Views: 2
Na Mwl John Pambalu

Nimeshangazwa sana na kauli ya mzee Kikwete aliyoitoa jana huko mkoani Mara siku moja baada ya tamko la Baraza la maaskofu Katoliki katika kile alichodai kuwa si sawa kuchanganya dini na siasa.

Kikwete ambaye marehemu Askofu Getrude Lwakatare alikuwa mbunge kupitia chama chake CCM na hakuwahi kuitoa kauli kama hiyo anayoitoa sasa. Kikwete ambaye Askofu Gwajima anayezunguka kuhubiri nchi nzima huku akitumia madhabahu kumnadi Rais Samia, wabunge na madiwani kwenye madhabahu na Kikwete alichagua kunyamaza. Kikwete ambaye Sheikh Mkuu wa Dar es laam Sheikh Walid Alhad aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Malezi wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Dar es laam, Kikwete alichagua kukaa kimya. Nini kinamtoa pangoni sasa?

Kwanza, upo uwezekano kuwa yumo kwenye scandal ya bandari kupewa waarabu so anatetea mkate wake wa kila siku.

Pili, anaona CCM chama chake kinaenda kuanguka kwa kukosa ushawishi kiasi kwamba sasa wanaogopa nguvu ya maaskofu katika ku speedup anguko la CCM kutokana na uovu wao.

Tatu: Unafiki.

Sasa wacha nimpe Darasa.

Mzee JK akimuona askofu ajue huyo askofu ameshirikishwa Ukuhani, Unabii na Ufalme wa Kristu. Leo nitazungumzia unabii tu na nitatolea mifano ya manabii wawili, Nabii Samweli na Nabii Nathani.

Zamani Mungu aliwatumia manabii kuwapaka watu mafuta ili wawe wafalme rejea 1 Samweli 9:17 "Huyu ndiye mtu niliyekwambia habari zake! Yeye ndiye atakayewatawala watu wangu". Hapa Nabii samweli anaambiwa amsimike mfalme Sauli kuwa nabii wa Israeli. Hii hata nchini kwetu huwa tunafanya, wakati wa kumuapisha Rais viongozi wa dini wanaalikwa ili washuhudie ama kushiriki kumsimika Rais mteule.

Hata katika kumkataa mfalme Mungu hutumia manabii Rajea 1 Samweli 16:1-7 "BWANA akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israel?". Samweli aliyetumika kumsimka Sauli kuwa nabii, Samweli yuleyule anatumiwa tena kuambiwa kuwa Mungu amemkataa Sauli.

Nafikiri unaweza ona namna dini na siasa zilivyokuwa zikihusika tangu Mwanzo katika kuwaweka na kuwaondoa wafalme.

Wakati fulani mfalme Daud alimchungulia mke wa mwanajeshi wake akioga yule mwanajeshi alikuwa akiitwa Huria. Akamtamani akalala na yule mwanamke, mwanamke akapata mimba, Daud akaagiza mumewe arejeshwe kutoka jeshini ili amlishe, amnyweshe na amuache akalale na mkewe ili ionekane ile mimba ni yake (Deception)

Mwanajeshi akarudi kweli akala na kunywa ila kwa kuwa alikuwa akijua miiko ukiwa vitani huruhusiwi kulala na mkeo hakwenda kulala na mkewe. Mfalme akakasirika akaagiza apelekwe kwenye mapambano makali vitani ili apigwe afe. Kweli akauawa vitani, mfalme Daud akamchukua mke wa yule jamaa.

Mungu akakasirika akamtuma nabii Nathani aende kumuonya mfalme Daud Rejea 2 Samweli 12:1-25 Mfalme Daudi akalia akatubu akisema, “Nimetenda dhambi dhidi ya Mwenyezi-Mungu.” Mungu akamsamehe akaendelea kutawala Israel.

Nataka kusema nini?

1. Kama Nabii Nathani (wa dini) alimuonya mfalme Daudi (wa siasa) dhambi iko wapi maaskofu kumkemea Rais Samia?

2. Kama Mfalme Daudi alijua makosa yake akanyenyekea na kutubu na kuacha njia yake mbaya, kwa nini Rais Samia asitazame nyuma na kuachana na mkataba ovu wa Bandari. Ili aendelee kutawala kwa amani bila pressure kutoka kwa umma wa anaowaongoza?

Nafikiri Rais bado anayo nafasi, asimsikilize Kikwete bali aangalie wapi kajikwaa, apige chini mkataba wa bandari, asimame tena asonge mbele akiwa na uhakika kuwa kama kuna mahali alifanya vibaya kwa hila, rushwa ama upendeleo Mwenyezi Mungu ni mwingi wa Rehema na Neema atamsamehe na kumuimarisha tena maana hatujakamilika huo ndiyo ubinadamu wetu.

La! akishupaza shingo maneno haya yatamuhusu. Arejee Daniel 5: 24-28 Ndipo kile kitanga cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya yameandikwa. Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI. Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha. TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka. PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.

Wasalaam
John Pambalu
Pretoria - Afrika Kusuni
21.08.2023
Umefafanua vizuri sana.

Kiufupi ni kwamba ama Kikwete haelewi au ameamua kuwa mnafiki.

Kwa mtu mwenye hekima japo ya kiasi kidogo sana, angeona haya kwa yale aliyoyatamka. Yaani maaskofu wa Kanisa Katoliki kutoa kauli dhidi ya mkataba wa hovyo anaona ni udini, lakini CCM kuwa na wabunge maaskofu na mashekhe kuwaingiza kwenye nafasi za kiutawala, haoni kama ni kuchanganya dini na siasa!! Ajabu sana.

Kiufupi, maneno ya Kikwete ambayo kimsingi hayana ukweli wala uhalisia, na ya kuopuuzwa ba kila mwenye uelewa.
 
Kwa Rais Mstaafu @jmkikwete na mnaosema Baraza La Maaskofu wana chuki za kidini. Naombeni mnieleweshe:

[emoji3578]Baraza hili la maakofu (TEC) mwaka 2018 lilipotoa waraka wa Pasaka wa kupinga mauaji na utekaji wa watu uliofanywa na Serikali ya Jiwe walikua na vhuki ya Kidini na 'Mkatoliki' Mwenzao Magufuli?

[emoji3578]Mmesahau Askofu Severine Niwemuguzi alinyang’anywa Passport na kuambiwa sio raia kwa sababu ya kupinga uonevu wa
Jiwe, alikua na chuki na Mkatoliki mwenzake?

[emoji3578]Wakati wa COVID Baraza La Maaskofu lilipotoa waraka wa kumpinga Magufuli kuwa COVID haipo na kutaka serikali iruhusu watu wapewe chanjo, walikua na chuki za kidini na Magufuli Mkristo mwenzao?

[emoji3578]Walivyo kemea madudu ya uchaguzi wa 2020 walikuwa na chuki za kidini na Magufuli Mkristo mwenzao?

[emoji3578]Kama kila wakati kukiwa na mjadala wa kitaifa wanatoa Waraka, na hamkuwai kuona shida, kwanini mnataka sasa wasitoe?

[emoji3578]Kwahiyo wakitoa kwa Mkristo mwenzao sio chuki? Wakitoa sasa kwa Muislam ndio wana chuki?
Sasa haya nayo si yangeambatanishwa kule nyuma ya waraka maana yameweka kumbukumbu sawa bin sawia.
 
Back
Top Bottom