Iselamagazi
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 6,020
- 6,161
Uko sawa kabisa kuhusu dialect!Mkuu nakushauri ukasome upya maana ya dialect kwa tafsiri nyepesi dialect ni utofauti mdogo mdogo unaotokea ktk matumizi ya lugha moja miongoni mwa watumiaji wa lugha hiyo.
Utofauti huo unaweza kuwa wa kimatamshi au kimisamiati au kimaana.
Mfano mzuri ni kiingereza,akizungumza mtu wa England ataeleweka na watumiaji wote wa kiingereza mfano mmarekani, mnaijeria na East Africa, South Africa nk. japo viingereza vyao havifanani hasa kwenye matamshi.Katika hali hiyo tunasema hizo dialect ni mutual intelligible kwa maana wanaelewana.
Kwa uchagani ni tofauti sana, mimi ni mkibosho na nakijua vizuri,akitokea mtu wa Rombo siwezi kumuelewa kabisa wala yeye hawezi kunielewa. Vivyo hivo Msiha na Mrombo au Mkibosho hawawezi kuelewana kabisa utofauti ni mkubwa mnoo. Tunaweza kusema ni lugha tofauti kabisa zinazotumika miongoni mwa Wachaga
In general hakuna kabila la Wachaga kama ilivyo kwa Wasukuma.
Hakuna kabila la Wasukuma!
Sukuma maana yake ni Kaskazini.