Wachaga ni moja ya kabila lenye dialects nyingi Tanzania

Wachaga ni moja ya kabila lenye dialects nyingi Tanzania

Mkuu nakushauri ukasome upya maana ya dialect kwa tafsiri nyepesi dialect ni utofauti mdogo mdogo unaotokea ktk matumizi ya lugha moja miongoni mwa watumiaji wa lugha hiyo.

Utofauti huo unaweza kuwa wa kimatamshi au kimisamiati au kimaana.

Mfano mzuri ni kiingereza,akizungumza mtu wa England ataeleweka na watumiaji wote wa kiingereza mfano mmarekani, mnaijeria na East Africa, South Africa nk. japo viingereza vyao havifanani hasa kwenye matamshi.Katika hali hiyo tunasema hizo dialect ni mutual intelligible kwa maana wanaelewana.

Kwa uchagani ni tofauti sana, mimi ni mkibosho na nakijua vizuri,akitokea mtu wa Rombo siwezi kumuelewa kabisa wala yeye hawezi kunielewa. Vivyo hivo Msiha na Mrombo au Mkibosho hawawezi kuelewana kabisa utofauti ni mkubwa mnoo. Tunaweza kusema ni lugha tofauti kabisa zinazotumika miongoni mwa Wachaga
Uko sawa kabisa kuhusu dialect!
In general hakuna kabila la Wachaga kama ilivyo kwa Wasukuma.
Hakuna kabila la Wasukuma!
Sukuma maana yake ni Kaskazini.
 
Kwanini wote waitwe wachaga huku hawasikilizani?ila kila koo kujikita katika upande wake nadhani umesaidia kuleta challenges baina yao na hivyo kuleta maendeleo.
 
Wachaga hawajali ukabila miongoni mwao ila muhimu maendeleo
 
Zifuatazo ni dialects za lugha ya Kichagga nyingine zinaendana
  • Kirombo
  • Kimarangu
  • Ki-uru
  • Kikibosho
  • Kimachame
  • Kisanya

Lugha zifuatazo zinauhusiano mkubwa sana na lugha za kichaga japokua wanajihesabia sio Wachagga.
  • Kimeru
  • Kigweno
Mfano: Msanya ni ngumu sana kumsema Mmeru, na Mmarangu ni ngumu sana kumsema Mgweno.
Pamoja na michango mingine ya wadau, hakuna lugha inayoitwa kimarangu. Marangu ni sehemu ndogo tu ya Vunjo na lugha unaizungumzia inaongelewa eneo lote la Vunjo.
 
Wachagga ni Taifa lenye makabila ya Rombo, Kibosho, Machame, Marangu nk.

Jina "Chagga" lilitokana na jina "kichaka" yaani watu walifyeka msitu na kuishi humo. Waswahili wakawatambulisha kwa Wakoloni kwamba hawa ni 'wachaka' yaani wanakaa vichakani.

Basi jina likazoeleka "Wachagga".

Kimsingi, mwanzoni jina "Wachagga" halikuwepo bali majina yaliyokuwepo ni Wamachame, Wakibosho, Wamarangu, Warombo, Wauru, Wamoshi nk. Na kila kabila lilikuwa na himaya yake na pia palikuwepo Mangi Mkuu ambaye alikuwa Kiongozi Mkuu.

Mpaka mwaka 1958, himaya ya Wachagga ilikuwa na bendera yake ambayo kwa Sasa ni bendera ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi. Pia ilikuwa na ikulu, ambayo ndiyo ikulu ndogo kwa sasa ya mkoa.

Pia palikuwa na Gazeti la Konkya, majengo ya utawala(kwa Sasa yanatumiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Moshi).

Pia palikuwepo na Chagga Democratic Party (CDP), na Kilimanjaro Development Council (Baraza la Maendeleo la Mkoa).

Mimi kwa maoni yangu, Wachagga siyo kabila bali ni Taifa dogo ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hivyo yaani!
Misifa kazini!
 
Back
Top Bottom