Wachaga tukutane mjadala wa mwisho wa mwaka

KING ASSENGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2016
Posts
928
Reaction score
1,478
Haika Ruwa,

Wachaga wote wa Rombo, Marangu, kirua vunjo, Wakibosho Wamachame, wa Huru wa Hai na pande zote, ikifika mwisho wa mwaka swali la kwanza ambalo tunajiuliza ni je, tumefikia malengo tuliyojiwekea mwaka huu?

Tufanye nini ili mwakani tuende mbele zaidi na kufikia malengo kirahisi zaidi? Umoja wa Wachaga katika miji, vijiji, mikoa na nchi mbalimbali unasonga ipasavyo?

Mchaga usisahau kurudi nyumbani.
 
Na zile ibada za mwisho wa mwaka... umesahau kuwakumbusha
 
Wachaga mnieleweshe kitu hapa aisee.
Inakuaje mnakua wachaga (kabila moja) halafu lugha tofauti kulingana na maeneo.??
Kuna jamaa yeye ni mchaga wa rombo na mwingine wa machame (kama sijakosea) nikashangaa kuskia eti hawawezi kuelewana coz lugha zao ni tofauti!!.

Au ni makabila mengi yaliungana ndo ukaundwa uchaga??
 
Hawa wamachame ndiyo wale wa kuua wanaume? Nasikia Kuna sehemu ukifika unakutana na wanawake wajane tu huko uchagani.
 
Jana nilikiwa naangalia kombe la dunia Kati ya England na Senegal, Senegal alipopoligwa la 3 mtangazaji alisema "Kuna muda unatakiwa ujifunze kutoka kwa waliofanikiwa badala ya kujenga chuki" akimaanisha kile kipigo Cha sisi weusi (Senegal) kiwe funzo kwetu badala ya kuwachukia wazungu kwa kuonyesha uwezo mkubwa.

Nikiwa mtanzania,nathubutu kusema wachaga ni moja ya kabila Bora Sana ambalo linapaswa kupigiwa mfano si bongo tu,Bali pia barani Afrika. Jamaa ni wapambanaji sana.Inadurahisha kuona jinsi wanavyonivunia kuwa wao,Ni Kama wamarekani wanavyonivunia kuwa wamarekani na kutembea kifua mbele duniani kote. Ukiwa negative huwezi kujifunza.
 
Mchaga hajawahi kuwa na mashirikiano ya kweli na dhati na asiye mchaga, jipendekeze ila mwisho atakubagua na atakusaliti tu na utajuta.

Hata mchaga mlokole ni mlokole wa mwili tu lakini sio nafsi na roho never.
 
Na wachaga wanaooa/kuolewa na makabila mengine hao unawazungumziaje??

Mfano mama mnyakyusa na baba mchaga watoto watakua pia wachaga, je watambagua mama yao.?
Huenda ulilosema ni kweli ila jaribu kuliweka vizuri, hata kama ni wabaguzi ila sio to that extent mkuu.
 
Labda wa kuoa 30% lakini wa kuolewa 1000% anabaki kwao na watoto mbegu yako atazaa labda mmoja, kimsingi hawezi kujiweka kama sehemu ya familia ya mume, nawajuq, nawafahamu, marry at ur own risk,
 
Jana nilikiwa naangalia kombe la dunia Kati ya England na Senegal, Senegal alipopoligwa la 3 mtangazaji alisema "Kuna muda unatakiwa ujifunze kutoka kwa waliofanikiwa badala ya kujenga chuki" akimaanisha kile kipigo Cha sisi weusi (Senegal) kiwe funzo kwetu badala ya kuwachukia wazungu kwa kuonyesha uwezo mkubwa.

Nikiwa mtanzania,nathubutu kusema wachaga ni moja ya kabila Bora Sana ambalo linapaswa kupigiwa mfano si bongo tu,Bali pia barani Afrika. Jamaa ni wapambanaji sana.Inadurahisha kuona jinsi wanavyonivunia kuwa wao,Ni Kama wamarekani wanavyonivunia kuwa wamarekani na kutembea kifua mbele duniani kote. Ukiwa negative huwezi kujifunza.

Neno!
 
Mchaga hajawahi kuwa na mashirikiano ya kweli na dhati na asiye mchaga, jipendekeze ila mwisho atakubagua na atakusaliti tu na utajuta.

Hata mchaga mlokole ni mlokole wa mwili tu lakini sio nafsi na roho never.

Ondoa uwongo wako hapa [emoji35]
Kama umechukia sana tafuna uwembe [emoji2959]
 
Labda wa kuoa 30% lakini wa kuolewa 1000% anabaki kwao na watoto mbegu yako atazaa labda mmoja, kimsingi hawezi kujiweka kama sehemu ya familia ya mume, nawajuq, nawafahamu, marry at ur own risk,

Uwongo wa hali ya juu sana, hayo mambo ni ya zamani sana,
Sasa hivi uchagani ni wasomi watupu, kwanza hamna hata sehemu kubwa ya kulima ambayo ndio ilikuwa sababu kubwa ya mke kubaki nyumbani!
Sasa hivi wanalima sehemu mbali mbali za Tanzania [emoji1241]
Na ni mashamba makubwa.
Kama una uwivu sana na wachaga nenda jinyonge walahi [emoji3062]
 
df1b8699-934d-42ea-8c7e-ef8952bc0861.jpg
 
Nawatakia wachaga wote uzima na furaha tele kipindi hiki kizuri cha sikukuu walahi!
Kusiwe na vilio wala maumivu ya aina yoyote!
Mwenye Enzi Mungu atuangazie uso wake na kutupa baraka zote na kubwa walahi!
Aaamina [emoji2972]
 
Back
Top Bottom