Baljurashi
JF-Expert Member
- Dec 30, 2017
- 1,628
- 2,720
Mbona povu? Kwani mzee Mohammed lengo lake lilikuwa ni kuandika historia yote ya wachagga? Lengo lake ni kuandika historia ya mzee Rajabu Kirama (Allah Amsamehe na Amrehemu) na labda historia ya Uislam Uchaggani.La
Labda nikusaidie labda kwa wasiotaka kufuatilia historia zao. Kwa mchagga yeyote historia yake ina zaid ya miaka mia nne coz yapo mashina yote yenye kuonyesha namna ukoo ulivyoanza mpaka na huyu mmiliki wa huo ukoo alivyouanzisha na umashuhur wake pale kijijin. So kupata historia ya kirama miaka hiyo sio yeye tu kila mtu uchaggan iko hivyo. Mwambie yeyote mchagga afanye utafiti koo zilianzaje. Na wale wazee walikuwa na shule kwa vijana ambazo ni alama kwa kwa kutumia fimbo. So hiyo umechukua history ya mtu ukaifanya ya wachagga. Pili miaka hiyo mangi ndio alikuwa mtawala na jaji so ukitaka chochote lazima uende kwa mangi so Kirama kwenda kwa mangi kudai kitu ni suala la kawaida kwa raia wa wakati huo sio jambo kuubwa. Mi Babu mzaa Babu yetu alikuwa nchili wa mangi Sina yaan mshaur so sikuambii vitu kwa kubahatisha. Nikipata muda nitakuwekea hapa namba ya mtu anaeuza kitabu cha historia halisi ya uchaggan. Kiuchumi kijamii na kisiasa. Acha hiyo yako ya kirama. Chagga land lilikuwa taifa kabisa Mzee sio hizo porojo zako za kuchagua cha kuandika. Tatizo lako unachagua pa kufanyia historia na watu wa kukupa historia. Hufanyi tafiti. Fanya jumla ya Mambo yote. Wachagga walitokea wapi wakafikaje tawala za mangi zilikuwaje kijamii kisiasa nk. Coz kuna mangi wakuu na wadogo. Kuna wachili kuna fumba kite kuna vipengele vingi mno ni kama utawala wa nchi ulivyosasa. Halafu uje shule na malumbo. Miaka hiyo kabla ya wazungu. Halafu mila na destur, miiko, vita na nk. Sasa wewe ukisimama ni kirama kirama kaleta uislam so what. Unajua wachagga walikuwa na baloz ujeruman nyakati za ujeruman inatawala nchi wewe. Na ni vigumu kuwatenganisha wachagga na kanisa maana mpaka kesho mafaili yapo namna kanisa likiwasaidia kupata elim. Japo kabla ya kanisa mfalme wa Zanzibar alikuwa na mahusiano mazur na mamangi maana alikuwa anatuma misfara inapita kwaajili ya biashara zake kiulinz. So kuna mengi hujui wewe endelea kuandika historia ya kirama maana hutakosa wa kumkamata. Lakin kwangu na kukatalia kama mwanzo. Huijui historia ya wachagga. Ungetuelezea hata historia ya Koo kubwa tu ningekuelewa. Na malumbo hivyo tu.
Na ushasema vitabu vya historia ya wachagga vipo. Sasa tatizo liko wapi? Mzee Mohammed kachagua kuandika ya Uislam huko uchaggani. Povu la nini?