Wachambuzi akina Jemedari Said na Ally Kamwe acheni Kujipendekeza Kinafiki kwa kusema Simba SC imeonewa na Refa wa Jana pale Afrika Kusini

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Leo Jemedari Said Kazumari bila hata Aibu (Haya) na ukiongozwa na Unafiki wako wakati Ukweli unaujua ukizingatia kuwa hata Mpira Umeucheza na unaujua vyema tu unasema Refa wa Jana ameionea mno Simba SC na Kuibeba Orlando Pirates FC.

Nakuomba rejea kutizama Mechi ya awali kati ya Simba SC na Orlando Pirates FC waliyocheza hapa Dar es Salaam kisha utagundua kuwa hata Sisi Simba SC tulibebwa na Kupendelewa na Refa katika Matukio mengi tu.

Na Wewe Ally Kamwe nimeona mahala ukisema kuwa lile Goli la Orlando Pirates FC lilikuwa ni Offside huku mkimlaumu Refa kuwa hakutaka kwenda Kujiridhisha katika VAR System.

Labda nikusaidie tu kama yule Mwamuzi (Refa) aliyechezesha Mechi ya Simba SC na Orlando Pirates FC hapa Dar es Salaam angesema ayafuatilie Matukio muhimu ya Kimchezo katika ile Mechi kuna uwezekano mkubwa hata ile Penati Simba SC tusingepewa na badala yake tungefungwa Goli za kutosha tu.

Na bahati nzuri Mimi MINOCYCLINE ninayewasema hapa ni 100% mwana Simba SC na siyo Yanga SC (Mabingwa Watarajiwa wa NBC Premier League 2021 / 2022) hivyo nawaombeni tu acheni Kuchambua na Kukosoa Kwenu huku kwa Kujipendekeza (Kujikomba) kwa Uongozi wa Simba SC (hasa CEO Barbara Gonzalez) ambaye Watu tunaofuatilia Mambo Magumu ya Taarifa tumehakikishiwa kuwa baadhi yenu Wachambuzi mpo katika Payroll za hivi Vilabu Vikubwa nchini na kwamba ukichambua kwa Kuwapendelea na Kuwasifia baadae unaona Salio Jipya la Pesa limeingia katika Muamala wa Simu yako (zenu)

MINOCYCLINE ninachojua ni kwamba Simba SC tumepambana Kadri ya Uwezo wetu na tumefungwa Kimchezo na kwa Mapungufu kadhaa ya Kiufundi niliyoyaona hivyo tusikate Tamaa, tujipange zaidi kwa Mashindano yajayo, tujirekebishe na tuendelee Kujifunza kwa Faida ya Mashindano yajayo, you ila hizi Ngonjera zenu kuwa Simba SC ilionewa nawaachieni nyie na Majuha (Mazuzu) Wenzenu kwani hakuna asiyejua kuwa Falsafa Kuu ya Mpira wa Afrika hasa katika Mashindano ya Kimataifa ni KILA MTU ASHINDE NA ABEBWE KWAO hivyo Refa alitubeba Nyumbani Dar es Salaam na Wao Refa kawabeba Kwao Johannesburg.

Imeisha hiyo....!!!!
 
Majuha( Mazuzu)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umepoteza nguvu na muda bure kujibu usichokijibu
 
Watanzania wana unafiki ulio tukuka na siyo kwenye mpira tu, angalia hata kwenye siasa. Simba imekuwa ikifaidika sana na uamzi wa marefa wanapokuwa uwanja wa nyumbani. Refa wa jana alikuwa very fair , ila Simba wajifunze uungwana wanapokuwa nyumbani vinginevyo ipo siku itawatokea ile ya Senegal vs Egypt .
 
popoma katika ubora wake...
 
Mbona hawajasema penalty aliyowanyima pirate? ONYANGO alishika mpira na Kuna beki pia kipindi Cha pili dk kama ya 88 akashika mpira ndani ya box. Kwa ujumla pirate wamenyimwa two clear penalty 😀.

Ujinga mmoja wapo wa watanzania na wachambuzi njaaa hawa ni kusahau kwao, Kuna watu mechi ya awali kwa mkapa walilalamikia refa kutokwenda kujilidhisha kwenye VAR baadhi ya wachambuzi na mbwigaziii zikasema sio lazima refa kwenda kwenye VAR kama ana uhakika na tukio husika!!.

Mlivyowanyonga kwa mkapa ndivyo mmenyongwa Soweto, muosha huoshwa!! Haya karibuni ligi mliyokuwa mnaiita ya matope.

Kingine kwa kocha hakuwa na uchaguzi mzuri wa kapteni kulingana na aina ya mechi, unampaje kitamba Cha unahodha mtu ambaye hawezi kufanya mawasiliano na refa?? Shabalala alikuwa yupoyupo tu hajui afanye nini kama nahodha!! Nahodha sio mvarishwa kitambaa tu ana jukum la kuwasiliana na refa.
 
Kwa ufupi simba amebebwa game zote mbili. Jana mabeki wawili wa simba wameshika mpira kwenye 18 lakini refa hakutoa penalty. Wakubali wameshindwa japo walipambana
Refa wala wasaidizi wake hawakuona na kamwe wasingeweza kuona sababu tushawaloga pale uwanjani kabla ya mpira kuanza.

 
Kuna mtu aliahidi kunya kuanzia stand ya Mbezi Hadi Msamvu, ukimuona nishtue
 
Refa wa jana anafaa kupewa medani sio kulaumiwa, angekuwa biased simba wangezama mapema mno kwa penalty
 
Kwa hiyo ulitaka waseme Pirates wamefunga goli lisilo la offside wakati limeonekana ni offside?
Mchambuzi akisema ukweli mnamkosoa akisema uongo mnamkosoa ,mnataka wakae kimya?

By the way huwezi kuwafurahisha watu wote duniani na hilo hata wao wanalifahamu vema
 
Una uhakika kwamba anajuwa kingereza? Maama labda tatizo ni ngeli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…