Wachambuzi msimwingilie kocha uchaguzi wa kikosi

Wachambuzi msimwingilie kocha uchaguzi wa kikosi

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Tanzania haijacheza finali za AFCON kwa miaka mingi kutokana na sababu nyingi sana. Mojawapo ya sababu hizo ni makocha wa timu ya taifa kushinikizwa uteuzi wa wachezaji.

Leo nilimsikia mchambuzi uchwara akihoji ni kwanini mchezaji fulani hakujumuishwa kwenye timu ya taifa iliyocheza na Sudan mechi ya kirafiki ya kimataifa, mchambuzi huyu ameanza kufilisika kichwani.

Kocha wa timu ya taifa anafuatilia wachezaji wote wa timu zote kwenye mechi zote. Tuache kocha afanye kazi yake ili tupate sababu ya kumfukuza badala ya kumshinikiza ampange mpwa wako. Komeni tabia hii ya kijinga.

Mfano, kuna mchambuzi anatokwa na povu kwanini Fei Toto aliachwa kwenye uteuzi badala ya kumtolea povu Fei Toto aongeze juhudi zaidi kiwanjani ili kocha amuone,
 
Kocha ameajiriwa kwa kodi zetu... Hivyo tuna kila sababu zakumwambia anapokosea!!. Kuhusu feisal huyo mchambuzi alipaswa kuchapwa viboko.
 
Tuna Wachambuzi TZ basi..?

We Wachambuzi kama Vile Vivulana Pale EA TV na EA Radio, huwa naona Vinatumia muda Mwingi Kubishana,wala Havijipi muda mmoja mmoja Kuchambua...!

Ipo haja Ya Ku set Criteria Za Mchambuzi Wa Soka awe na Standards Zipi..? Kwa sasa ni Vulugu Mechi...

Toka Mwl Tigana Aondoke Pale East Africa TV na Radio imekuwa tatizo....!
 
Kocha Adel ni kocha Bora tumefuzu Afcon ni vizuri aachwe afanye anavyojisikia, achague na kupanga wachezaji anaowataka, nimefurahi kamuita majogoro , muda wa timu kucheza Kwa majina umekwisha!
 
Back
Top Bottom