kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Vijana Wana kesho nyingi sana waacheni watembee polepole kuepuka kujikwaa.
Timu kubwa zina Zina mabenchi Bora ya ufundi na vitendekeakazi vingi, hivyo vina jukumu la kuibua vipaji vipya kwenye michezo ili kuziba nafasi za wanaozeeka. Wachambuzi Wana tabia za kuwajaza vichwa na kuwapandisha mabega vijana wetu wanaojitahidi kuzingatia mafunzo ya walimu wao uwanjani kiasi Cha kuwaogopesha walimu na wamiliki wa timu wanaotaka kuwekeza kwa vijana wadogo.
Mchezaji akijaribiwa na mwalimu wake kwa kupewa nafasi ya kucheza akionekana ameyashika mafunzo na kucheza kandanda safi kwenye mechi 2 basi vichambuzi uchwara vinajitokeza na kuvisikia vikisema ooo kaupiga mwingi sana, ni tegemeo la timu, anastahili malipo zaidi, hastahili kucheza timu Ile, anafaa kwenda Ulaya mapema, ooh wanampunja na upuuzi mwingine kibao. Hii tabia itawafanya makocha na wamiliki kukimbilia kununua wachezaji wakubwa TU (ready made players) kukwepa fedheha na kelele hizi,
Kijana akishawasikia wapuuzi wale basi nae tamaa ya utajiri wa haraka haraka inamjia na kuanza kuwa kama mgema kulitia tembo maji.
Wachambuzi wetu mnatusaidia sana kwenye tasnia ya michezo, lakini kabla ya kuzungunza jambo fikiria kwanza matokeo (impact) yake.
Vijana ni kundi ambako liko volatile, linataka matokeo ya leoleo na Sasa Sasa ndio maana wanapotea haraka sana kwenye ramani.
Vijana wetu wacheze mpira mwingi ili walimu wawaamini na kuwapa nafasi. Wakishapata hiyo nafasi wawe consistent kwenye ubora Huku wakiendelea kujitunza wasiumie mara kwa mara. Lazima timu kubwa zitawaona tu na kuwalipa fedha nyingi. Kijana kupata nafasi ya kufundishwa na kocha mkubwa wa timu kubwa na bahati kubwa sana, shukuru Mungu kupata bahati hiyo, ifanyie kazi kwelikweli, acheni kudanganywa na wachambuzi wasiokuwa na maudhui