Wachambuzi wa michongo tunaomba mrudie hesabu zenu

Maana hiyo ES Setif ipo nafasi ya 9 kwenye jedwali la msimamo wa ligi kuu ya soka ya Algeria. Etoil du Sahel inaburuza mkia kwenye ligi yao inayohusisha makundi.
Sasa mimi namuuliza unao uhakika hivyo vilabu vilivyo juu ya Simba SC vitamaliza top 2 kwenye ligi yao mpaka afikie hitimisho kwamba nafasi ya Simba SC haipo kwa kuwa miongoni mwa vilabu 10 vitakavyoanza First round instead of preliminary round of CAF. CL?

0.5 FC mmoja anijibu hapa.
Huyo Etoil du Sahel inabuluza mkia kwenye ligi ya wapi? Embu kaangalie vyema msimamo. Kuhusu Setif hata sikuizungumzia kabisa kwasababu yupo chini nafasi ya 13 pamoja na Simba. Tukija kwenye swali lako ulilouliza kuhusu swali lako la msingi la huko juu ni kwamba mpaka sasa

# Kati ya Al Ahly, Pyramid na Zamalek wanaweza timu mbili kati hizo tatu zinaweza kucheza klabu bingwa kutokana na msimamo wa ligi yao ilivyo. Yeyote atakayeingia hapo atakuwa na uwezo wa kuanzia raundi ya pili kwasababu tumu zote tatu zimemzidi Simba point.

# Tp Mazembe anaongoza ligi yao
# Petro luanda anaongoza ligi
# Whydad na Raja Casablanca mmoja anaongoza mwingine ni wa pili
# Mamelod anaongoza ligi
# Horaya anaongoza ligi
# Es Tunis anaongoza kundi kwenye ligi yao
#Etoil de Sahel anashika nafasi ya tatu kwenye kundi lake na sio kama ulivyodanganya wewe kuwa anaburuza mkia

IMG_20220424_112845.jpg
 
Mkuu,hili swali lako limemaliza huu mjadala tayari,hapa umemshika pabaya na hawezi kamwe kujaribu kujibu.
Pole sana mtag mwambie kaishajibu na uthibitisho umeletwa mwambie aje nayeye alete uthibitisho unaonesha Etoil du Sahel anabuluza mkia.
 
Sasa huyo wa tatu anakwenda wapi na yupo nafasi ya tatu huko kwao? Au tu atacheza CL kwakuwa anaizidi Simba point kwa mujibu wako[emoji4]
 
Duh mmeahama hoja kutoka kwenye kuburuza mkia mpaka kwenye wa tatu anaenda wapi. Haya ela ya ada mnatoa sh ngapi niendelee kutoa darasa kwako na yule brother K (wakukurupuka)uliyekuwa unamshingilia kwa kusema Etoil du Sahel wanaburuza mkia? Kumbe hata mfumo wa ligi ya Tunisia haujui wanaendeshaje ligi yao.
 
Wewe jibu hoja,unazunguka nini? Btw tunafanya huu mjadala kwakuwa Simba ipo katika hiyo level,kusingekuwepo na mjadala kama huu endapo Simba ingekuwa kama wale wa Kawaida Utopolo huko
 
Kama wale wenye 0.5 hawataanzia kwenye level anayoanzia Simba Sc, badi hakuna shida yoyote sisi kama Simba Sc, tutafurahi.
 
Mkuu ngoma ipo 50/50 inaweza tokea kuanza nao kwenye level moja kitokana rank aliyonayo Simba mpaka ame drop hadi nafasi ya 13 hivyo maombi yenu ni timu tatu zilizo kwenye nafasi ya kwanza hadi ya kumi zishindwe kufuzu kwenye ligi zao ili zari liliwaangukie nyie.
 
Wewe jibu hoja,unazunguka nini? Btw tunafanya huu mjadala kwakuwa Simba ipo katika hiyo level,kusingekuwepo na mjadala kama huu endapo Simba ingekuwa kama wale wa Kawaida Utopolo huko
Ipo hivi ligi ya Tunisia wao huwa wanaanza kwa kupanga makundi mawili kundi A na kundi B kisha zinachukuliwa tumu tatu bora kwenye makundi yote mawili na kufanya timu ziwe sita ambazo zitashindanishwa wenyewe kwa wenyewe.

Kumbuka kuelekea hatua ya mwisho ambayo ni play off, timu zilizoongoza kundi anapewa advantage ya kuongezewa point 3 na aliyeshika nafasi ya pili anapewa +2 na aliyeshika nafasi ya tatu anapewa +1
 
Mkuu ngoma ipo 50/50 inaweza tokea kuanza nao kwenye level moja kitokana rank aliyonayo Simba mpaka ame drop hadi nafasi ya 13 hivyo maombi yenu ni timu tatu zilizo kwenye nafasi ya kwanza hadi ya kumi zishindwe kufuzu kwenye ligi zao ili zari liliwaangukie nyie.
Kikubwa ni kwamba, kwa wale 0.5 fc ni uhakika kuanzia mbali huko ila kwa Simba Sc bado haijukilikani.

Kwa waliosoma hesabu:

Probability ya Yanga kuanzia hatua ya awali ni = 1

Probability ya Simba kuanzia hatua ya awali ni <1.

Hivyo sio sawa kusema kuwa ni 50/50.
 
Humu kuna hesabu za uongo na kweli watu wakipeana imani kuwa simba ina uhakika ya kuanzia raundi ya pili kwasababu anashika nafasi ya 12 hivyo ana uhakika wa kuchukua nafasi ya pyramid na Berkane msimu ujao endapo watatolewa na Pirates hapo kesho. Wachambuzi wa bongo wameangalia tu upande wa juu ya Simba na kutoa hitimisho lakini kwasasa mambo yameshabadilika huko simba ili waanze raundi ya pili msiku ujao ni lazima kesho wamtoe Orlando pirates maana hakutakuwa na mbeleko ya Berkane wala Pyramid. Mpaka sasa msimamo upo hivi

1) Al Ahly point 73
2) Esperance point 58
3) Wydad point 56
4)Raja point 54
5)Mamelod point 46
6) Zamalek point 43
7) Berkane point 39 huyu namtoa kwasababu hatofuzu hivyo nafasi yake inabebwa na [emoji116]
7) Tp Mazembe point 38
8) Pyramid point 34 huyu nae hatofuzu hivyo namtoa pia hivyo yake itabebwa na [emoji116]
8)Pdtro luanda point 33
9) Etoil du Sahel point 32
10) Horoya point 31
11) Simba & Setif wote point 28

Timu ya kwanza hadi ya kumi zote zina uhakika wa kufuzu kwenye ligi zao kucheza klabu bingwa. Hivyo njia pekee ya Simba kutoanza hatua ya awali ni kumtoa Orlando pirates kesho
Ni vyema sana ukamuonesha Haji Manara hii post yako
 
Kikubwa ni kwamba, kwa wale 0.5 fc ni uhakika kuanzia mbali huko ila kwa Simba Sc bado haijukilikani.

Kwa waliosoma hesabu:

Probability ya Yanga kuanzia hatua ya awali ni = 1

Probability ya Simba kuanzia hatua ya awali ni
Hivyo sio sawa kusema kuwa ni 50/50.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kikubwa ni kwamba, kwa wale 0.5 fc ni uhakika kuanzia mbali huko ila kwa Simba Sc bado haijukilikani.

Kwa waliosoma hesabu:

Probability ya Yanga kuanzia hatua ya awali ni = 1

Probability ya Simba kuanzia hatua ya awali ni
Hivyo sio sawa kusema kuwa ni 50/50.
Hivi mfano timu ikichukua kombe la klabu bingwa lakini nchini kwao imeshindwa kufuzu, je ataruhusiwa kucheza klabu bingwa kama bingwa mtetezi?
 
Inangia kama mtetezi, na hata akichukua CAFCC kisha asimalize kwenye zile nafasi za juu kabisa bado atakuwa na sifa za kuingia.
 
Ngoja tuone mwaka huu kutakuwa maajabu yapi maana msimu uliopita tumeona timu mbovu ikicheza fainali dhidi ya Al Ahly. Sijui msimu huu kitajili kipi
 
Ipo hivi ligi ya Tunisia wao huwa wanaanza kwa kupanga makundi mawili kundi A na kundi B kisha zinachukuliwa tumu tatu bora kwenye makundi yote mawili na kufanya timu ziwe sita ambazo zitashindanishwa wenyewe kwa wenyewe.

Kumbuka kuelekea hatua ya mwisho ambayo ni play off, timu zilizoongoza kundi anapewa advantage ya kuongezewa point 3 na aliyeshika nafasi ya pili anapewa +2 na aliyeshika nafasi ya tatu anapewa +1
Sasa kama ni hivyo basi huyo wa tatu bado ana wakati mgumu sana kwenye play off.Hata hivyo nashukuru sana kwa hii informative comment.
 
Back
Top Bottom