Wachambuzi wa mpira wa kibongo na ujuaji bila kucheza mpira

Ladder 49

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
7,918
Reaction score
20,037
Wakuu habari zenu,nimeachakuwasikiliza hawa wachambuzi wa kibongo wa mpira

Nitawasikiliza kama ni kocha wa mpira au mchezaji kama hajawahi kucheza mpira,Sipotezi kumuda kumsikiliza,(ulaya wachambuzi wanaochambua mpira walishacheza mpira ligi zinazoeleweka ).

maana wenyewe wanakuambia hawana timu sasa kama hawana timu wanaangaliaga mechi gani?

Haya kama wanatimu ila ni siri yao,sasa uwezo wakuzijua hizo timu zingine wanautoa wapi? Maana hawajanizidi kwa kuangalia mechi za timu yangu ambayo ni tofauti na timu yake anayosema ni siri yake,

Mfano me ni shabiki wa Liverpool mechi zote za Liverpool lazima niangalie hata kama anacheza na timu ndogo

Nauwezo wa kuijua timu yangu,yeye aangalii mechi zote baadhi tu ndio anaangalia

Halafu mwisho wa siku anakuja kukuambia uchambuzi wake timu yako itafungwa kwa sababu ya moja mbili tatu na wakati wewe timu unaangalia mechi zote hata iwesaa kumi na moja ya asubuhi (mechi za preseason) lazima uangalie

Nimeachakuwasikiliza wachambuzi wasio na tahaluma ya ukocha na wasio cheza kwenye ligi kuu.

Jana nilikuwa nasikia kwenye radio mchambuzi mmoja anawauliza wenzake vipi mechi ya man city na Liverpool unabet wapi hiyo? Mmoja akajibu weka lazima kutakuwa na magoli mengi hiyo mechi hawatokagi draw bila ya goli.

Msimu uliopita walikutana mechi 4,kwenye mechi hizo kumekuwa na goli 18,

Nimeangalia mechi imeisha Liverpool vs man city wametoka sare ya bila ya kufungana hata goli yaani 0-0.

Sasa najiuliza hivi wanakuwaga wanafatiliaga hizo mechi za timu husika au wanaogea tu kwa mazoea? Nimeachakuwa sikiliza
Nawasilisha.
 
Kuwa mchambuzi hakuhitaji uwe umecheza mpira kuwa kocha hakukuhitaji uwe umecheza mpira kwa viwango vikubwa, mfano mzuri Joseph Blatter hajawahi kucheza mpira level kubwa na kaiongoza FIFA miaka mingi
 
Bongo wachambuzi vigeugeu,kabla ya game anasema hivi,baada ya game anakula matapishi yake
 
Labda ieleweke tunapokuwa tunachambua haimaanishi lazima iwe hivyo na hiyo ni dunia nzima wewe unadhani Barcelona alivyotolewa na Roma ni mchambuzi gani angebashiri Roma kumtoa Barca akiwa tayar kashinda 4-1 nyumbani
 
Sasa hapo anakuwa achambui mpira yeye anatabiri tu,

Mechi ya Roma vs Barcelona,goli 2 roma walijifunga wao wenyewe na Barcelona hiyo mechi walizidiwa sio ile Barcelona tunayoijua.
 
hakuna mahusiano ya moja kwa moja kati ya kucheza mpira na kuchambua mpira, kama ilivyo hakuna mahisiano katika ya kucheza mpira na kufundisha mpira. Kila kimoja ni fani inayojitegemea wenyewe kabisa. Acha mihemko mleta mada.
 
Mkuu inaingiaje hapo hiyo kucheza mpira na kufundisha mbona kama nje ya mada hiyo.

Kufundisha lazima uende shule na lazima ukaenatimu kama Jose mourihno alivyoenda Barcelona kujifunza

Mkuu yaani wewe ucheze mpira halafu kuelezea mbinu za Mwalimu ushindwe (wewe unafanya hiyo kazi ya uchambuzi) na asiyecheza cheza mpira yeye ndio anajua mbinu vizuri na kuelezea?

Hakuna kitu kama hicho.
Wasiocheza mpira wanakuwa na maneno mengi tu yasiyokuwa na maana ambayo wewe utayaita ndio uchambuzi wenyewe Ulaya wachambuzi wengi ni wachezaji hawawezi kukualika wewe uchambue mpira na wakati ujacheZa na ujasomea hiyo kitu wewe ni maneno tu matupu.
 
wachezaji wazamani ulaya wanapata priority kwa umashuhuri wao na sio vipaji. Hata makocha ndio huvo hivo ni rahisi kwa ma football legends kupata vibarua.

Narejea tena uchambuzi wa soka ni kipaji cha ueleo wa mpira na sio kuwa umecheza football, watizame Rio Fredinand na Gary Neville wakichambua one tope zao wanazozungumza.
 
Niwe tu mkweli nikitaka kusikia uchambuzi wa mpira huwa nawasikiliza Ally Mayai na Amri Kiemba basi ila nikitaka ushabiki na soga za mpira ndio nasikiliza hizo takataka nyingine

Back
Top Bottom