Wachambuzi wa Soka kuwa na mafanikio zaidi kuliko wachambuzi wa siasa

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Vipindi vya michezo vimekuwa vingi kwenye televisheni na radio licha ya kuwa vingi ni miongoni mwa vipindi vyenye muda mrefu; kwa makadirio vinachukua muda wa masaa mawili mpaka matatu kwa msingi huo usishangae kila kijiwe story zikiwa Simba na Yanga, Dewji na GSM, Ntibanzokiza na Mayele.

Wachambuzi wa soka wamekuwa wengi na wenye mafanikio in terms of Majina yao na Financial status zao. Twende kwenye facts Soka linagusa sehemu ya maisha ya watu wachache kulinganisha na siasa ambayo inagusa maisha ya kila mtu katika hali ya kawaida ilipaswa siasa ijadiliwe sana na ipewe airtime kubwa na pawepo wachambuzi wengi wa kisiasa ambao watatoa mapendekezo yao yatakayopelekea serikali kuchukua hatua zitakazoleta tija kwenye maisha ya kila Mtanzania.
 
Tatizo wachambuzi wasiasa waliendekeza njaa na ushabiki binafsi wa vyama ili wapete teuzi.
 
Kuliko kuchambua siasa ni heri niende Taifa nikaangalie mechi ya Simba au Yanga by the time.

Maana siasa zetu ni maudhi hasira na kero.Mwisho upate vidonda vyatumbo.

Mfano;Treni ya Umeme Dar Moro mpaka wa leo imekuwa hadithi na ahadi lukuki kila Mara.

Na hata yale Mabehewa mapya sijui yameishilia wapi?

Ni bora tukaangalie mpira huwenda vikatufariji
 
Siasa haipati Airtime ya kusikilizwa sana sbb ina haribu mood sana, binafsi sio siasa hata taarifa ya habari wala bunge sisikilizi.
Pamoja na kuharibu mood lakini ndiyo uhalisia wa maisha ulipo. Mpira ni furaha ya muda mfupi then unarudi kwenye shida zako za kila siku.
 
Kuliko kuchambua siasa ni heri niende Taifa nikaangalie mechi ya Simba au Yanga by the time.

Maana siasa zetu ni maudhi hasira na kero.Mwisho upate vidonda vyatumbo.

Mfano;Treni ya Umeme Dar Moro mpaka wa leo imekuwa hadithi na ahadi lukuki kila Mara.

Na hata yale Mabehewa mapya sijui yameishilia wapi?

Ni bora tukaangalie mpira huwenda vikatufariji
Imagine kama walau nusu tuu ya watanzania wangekuwa bize na kufuatilia siasa na wanasiasa na kukomaa nao kama wanavyokomaa na mpira unadhani hizi longo longo zingekuwepo? Hata viongozi wangeogopa kutoa ahadi za uongo na kula mali za umma.
 
Kuliko kuangali bunge bora uangalie cartoon na mwanao!! Siasa za kina msukuma ni Zaid ya uharo
 
Kuliko kuchambua siasa ni heri niende Taifa nikaangalie mechi ya Simba au Yanga by the time.

Maana siasa zetu ni maudhi hasira na kero.Mwisho upate vidonda vyatumbo.

Mfano;Treni ya Umeme Dar Moro mpaka wa leo imekuwa hadithi na ahadi lukuki kila Mara.

Na hata yale Mabehewa mapya sijui yameishilia wapi?

Ni bora tukaangalie mpira huwenda vikatufariji
Sasa Changomoto kama hizo ndio zinabidi zipigiwe kelele kwa lengo la kuwafikia wahusika
 
Imagine kama walau nusu tuu ya watanzania wangekuwa bize na kufuatilia siasa na wanasiasa na kukomaa nao kama wanavyokomaa na mpira unadhani hizi longo longo zingekuwepo? Hata viongozi wangeogopa kutoa ahadi za uongo na kula mali za umma.
Na hilo ndio jambo la msingi waheshimiwa wanashtuka mfano mzuri ni sakata la bandari lilivyojadiliwa na wengi limetuma ujumbe kwa viongozi kuwa WaTanzania wapo macho.
 
Back
Top Bottom