Wachambuzi wanaoleta Takwimu mbovu za Kocha mpya Yanga

Ameshinda nini cha maana mpaka kuwa kocha mzuri?
 
Bandiko limekaa kimpira zaidi kuliko ushabiki. Sijui wachambuzi wamejifunzia wapi hiyo taaluma. Wanaendeshwa zaidi na utimu kuliko facts.
 
Binafsi namuombea heri katika majukumu yake mapya. Kutimuliwa kwa Gamondi kulikuwa ni kwa kujitakia. Hivyo asitafutwe mchawi.
 
Mbona mnajieleza sana😆
 
Tunamuunga mkono na uongozi pia.
 
Chikola anamsalimia sana kocha wenu mpya kasema niwape ujumbe mumfikishie salamu.
 
Mpira wa bongo hautagemei kocha Sana unataka rushwa ndio maana ukitaka kutupima vizuri na Mpira wetu tupeleke kimataifa utaona povu linapotutoka utakuta huyu anasema kafika robo mara kavaa medali waulize vikombe vya CAF hawana
 
Huwezi kuwalaumu wachambuzi hasa kuhusiana na daraja wanalompa Sead Ramovic kwa kutumia rekodi zake, kwani ndivyo uwezo wa kocha unavyopimwa.

Pia, hukumu ya wachambuzi inampata kutokana na kocha anayemrithi, ni kama Yanga wametoa bunduki wakaweka kirungu. Kwani Gamondi ni bora kuliko Ramovic.

Ramovic ni kocha mchanga sana kwa Gamondi aliyepata mafanikio katika ligi kubwa za Afrika, akitwaa mataji na kujenga timu zisizofungika kirahisi uwanja wa nyumbani.

Mafanikio ya Ramovic ni kucheza kufikia fainali ya Carling Knockout Cup. Kwa daraja la Yanga, huyu kocha ni kama amekuja kujifunza uzoefu kupitia Yanga.

Ova
 
Basi Mmekwisha Utopolo vipigo mfululizo vitawahusu
 
HAKUNA KOCHA MBOVU WACHEZAJI NDIO KILA KITU,

MIMI NACHUKUA UBINGWA EPL NIKIWA NA KIKOSI CHA ARSENAL AU MANCITY.

GAMONDI AU GADIOLA UKIMPELEKA PAMBA INASHUKA DARAJA.
 
Kama wachambuzi wanazingua kuleta takwimu mbovu ni jukumu lako kuleta takwimu nzuri ili uwafunge mdomo.😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…