Wachambuzi Wanashiriki kuharibu future ya Sports

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wakuu,

Tumewazungumzia sana kizazi hiki cha wachambuzi wetu ambacho pia kinachangia kuharibu mpira wetu na hasa michezo isiyo soka alafu wao ndio mabingwa wa ulalamishi kwenye media zao. Yapo maeneo waliyofanya vizuri lakini sitaki kugusia huko.

Kuna kelele nyingi zilizoanza jana juu ya usajili wa Simba& Yanga zinazochochewa na habari hewa za wachambuzi wetu kwa staili ya copy and paste. Kila mchambuzi anajaribu kutaka kuonesha ana "exclusive" kwa habari za kihuni tu zisizo na source au hata kuandikwa kiweledi.

Nchi majuzi imetia aibu kwenye Olympics lakini si issue kwao zaidi ya kugusia kwa juu juu tu lakini mambo ya umbea wa usajili ndio wamejikitita tena wakirudia yale yale! Hivi hao wachezaji wanaowaniwa ni habari mpya? Nendeni kwenye page zao habari hiyo wanapost hadi leo kama kitu kipya! Ushabiki tu!

Tuna tatizo kubwa la creativity na udhubutu. Mfano mdogo ni miaka ya nyuma akina Masoud Masoud kule radio uhuru walibuni kipindi cha miziki ya zamani tena ile ya akina Mbaraka Mwinshehe, Juwata jazz band n.k kikavutia watu sana hadi radio zote zikaanza program ya vipindi hivyo ikiwemo Clouds! Baadae hizo program zimekufa! Sababu walitembea na upepo na si vision.

Kwanini michezo mingine inazungumzwa kwa staili ya kuzugazuga ili kipindi kisionekane ni soka tupu? Kwanini hatuwajibishani kwa kuelezana ukweli hata kwenye michezo kwa aibu ya Olympics?

Umbea umbea wa kipumbavu ndio Big ajenda sababu mnautengeneza wenyewe nyie wachambuzi alafu mnataka kutuaminisha ndicho wanachotaka wananchi. Shirikishoni kuna mgombea mmoja tu kwa namna ambayo ni very questionable lakini who cares?

Asilimia kubwa ya hawa wachambuzi wapo kwenye mainstream media maana yake ndio wanaoamua jamii ilishwe nini! Lakini nao wapo kwenye mazogo ya vijiweni!

Shame on you!
 
Haha
Pole,
Iwenyewe wanataka kutrend! Kumbuka ni wachambuzi na sio wana habari, mfano kitenge ana weledi wowote wa kiana habari?
Wanaandika habari za kuokota okota maana ndio zenye followers wengi, mfn banda kuchukuliwa na Yanga juu juu
Same na Aucho
 
Wanaharibu michezo hawa ..
 
I told you guys. Angalia uongo kuhusu msemaji wa Simba ulivyosambaa kwa kasi! Purely unprofessional.
 
Hizo ni habari za kiudukuzi, na Lisemwalo lipo kama halipo linakuja
 
Watoe humo George Ambangile Ali Kamwe na Jemedali Saidi hawa jamaa wanajua sana,, wengine waliobaki wajifunze na wabadilike wanakera sana,,
 
Hizo ni habari za kiudukuzi, na Lisemwalo lipo kama halipo linakuja

Bora leo hujatumia lugha ya Malkia kama kwenye uzi ule mwingine [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mambo mengine naona ni ya kujitakia tu! Hivi huwa mnalazimishwa kuwasikiliza hao wachambuzi?

Hakuna kitu kingine cha kusikiliza mpaka uwasikilize ili baadae uje ulalamike? Hivi Watanzania kulalamika ni ugonjwa wa kurithi, au!!

Yaani ccm ituvuruge, na wachambuzi wa michezo nao watuvuruge kweli!!! Tubadilike bhana!!
 
mkuu unahaha kama Ngolo kante kila uzi unaolalamimika matakataka ya redioni naona unajitahidi kutetea, ajabu sana hii
 
Wacha-mbuzi

Sijui nani alitafsiri kutoka neno PUNDIT
 
Ilipofikia sasa naamini menejimenti na mashabiki wanatakiwa wafanye kitu juu ya aina hii ya Waandishi na hawa wanaojiita ‘Wachambuzi’.

Kwanza wengi wao ni ‘empty set’ na bila habari za Simba hawawezi kuishi.

Ikibidi wazuiwe kutangaza habari zozote zinazoihusu timu ya Simba ili tuone hivyo ‘vipage na viyou tube’ vitafika wapi.
 
simba management nao wamezidi kuishobokea sana efm
 
I told you guys. Angalia uongo kuhusu msemaji wa Simba ulivyosambaa kwa kasi! Purely unprofessional.
Wewe umejuaje kama ni Uongo? Mbona Uongozi wa klabu hautoki hadharani kukanusha taarifa wakiwa na vielelezo.
 
Tatizo kuna timu badala ya kugundua haziwezi kushindana ndani ya uwanja zimeamua kuwekeza kwenye propaganda zikitumia waandishi na wachambuzi uchwara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…