WACHAPISHAJI WA VITABU

WACHAPISHAJI WA VITABU

Drat

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,160
Reaction score
1,359
Natumaini wote mnaendelea vizuri?

Kwa heshima na taadhima naombeni kama kuna mwandishi au mchapishaji anisaidie kupata mchapishaji wa vitabu kwa bei nafuu,yaani anipe mapendekezo ya wachapishaji kadhaa ambao ni very affordable.

Lengo ni kutoa vitabu vyangu viwili nikiwa huru, yaani nitauza mwenyewe.
 
Natumaini wote mnaendelea vizuri?
kama kuna mwandishi
Wakati tukisubiria michango toka kwa wadau wa vitabu.

Kuna waansishi Ndugu:
Yericko Nyerere
Makirita Amani

Hawa Members nilio wataja, Taayari wamemepitia hiki unachokipitia kwa sasa, Na wanavyo vitabu kadhaa vilivyochwapwa, Omba msaada kwao wakupe ABC, Na hakika utapata mahala pa kuanzia.

Kila lakheri Ndugu.
 
Bajeti yako ni kiasi gani, ungependelea kila kitabu kichapishwe kwa kiasi gani, na kina kurasa ngapi?
 
Kama umeshatengeneza cover page, una ISBN ambayo inapatikana maktaba ya taifa kwa 20k..

Itategemea kama unataka kitabu kisajiliwe COSOTA kwa ajili copyrights ambayo gharama zake sidhani kama inazidi 50k kwa kila kitu

Kuhusu bei, vitabu vinatofautiana kwa ukubwa kwa kuangalia ina pages ngapi lakini pia urefu na upana wa karatasi zake

Kama utaprint kwa A5, inakuwa cheaper ambacho kitabu cha page 100 kinaweza kisizidi 5,000 ila kwa jinsi unavyoongeza copies unazochapa na ndivyo bei inavyozidi kinapungua.

Printers ni wengi kariakoo hivyo lazma upewe direction ni wapi uchapishe kwa ajili ya ubora 🙏🏽
 
Back
Top Bottom