Wachawi wa elimu yetu ni hawa

Wachawi wa elimu yetu ni hawa

mimi nilisoma Bsc ed kwasababu niliupenda ualimu kuliko dentistry niliyoomba na nikaipata.

Kwa nini uliomba kitu ambacho hukuwa unakipenda? ambacho baadaye ukaacha kukisoma? Hukua na uhakika? Kiukweli najua wapo walimu ambao wako vizuri kitaaluma kama wewe na wengine wachache, lakini ukweli lazima usemwe na ubaki palepale (ukweli utasimama) waliowengi wametelezea huko baada ya kushindwa maeneo waliyoyataka. Tunashukuru kwenu ninyi wachache ambao ufaulu wenu ni mzuri na mkaamua kuingia huko.

Kama serikali ikaamua kwamba kusoma ualimu isiwe ''adhabu'', tutainua elimu yetu na HILO NDO LILIKUA WAZO LANGU KUU KATIKA MAELEZO YANGU YOTE maana malipo ya walimu ni duni na ndicho kinachopelekea watu wanaofanya vizuri katika mitihani yao wasipende kusoma ualimu, ''wachache kama ninyi mmejitolea'' Big up.
 
sikuomba kwa kubahatisha, zamani ilikuwa unaomba kusoma chuo kutokana na umesomea nini Alevel, nilipokwenda muhimbili niliupenda sana udaktari ila sikupenda mazingira ya kusomea na niliboreka na aina ya shule yenyewe.

so bado muhimbili ilikuwa ni tawi la UDSM nilikuja kwa CADO enzi hizo nikaomba kusoma general science kumbuka kabisa wakati wa zamani wengi wetu tulikosa watu wa kutuguide kwenye masomo yetu ya vyuo. nilipokuja namshukuru sana Prof Nkunya alinishauri kwamba nisisome general science as haina bright future kama ilivyo dentistry. lakini akasema kama sipendi kusoma tena dentistry basi soma BSC ed at least ukimajor biology na chem utakuwa na future nzuri sana.

ukweli namshukuru sana huyu baba, alitumika kunifanya nione maisha marahisi sana ingawa shule ya ualaimu kwa sayansi haikuwa rahisi, hasa kemia ilikuwa ngumu sana sana. lakini nimeona kwa kuwa mwl wa sayansi niliweza kujiendeleza na mpaka sasa ni mwl lkn nafanya kazi kama environment toxicologist and lab scientist.

sipendi jinsi ambavyo watu huona kaa fani ya ualimu ni ya watu waliokosa pa kwenda, kwani sio kweli wengi huwa tunaingia tukiwa na tegemeo la ajira mkononi ila huko kwenye ajira yenyewe ndiko kunako katisha tamaa na kutufanya wengi wetu kuchepuka kwenye fani nyingine.

Kuna mambi ambayo naomba Munu yarekebishwe kwenye ajira ya ualimu, na kama ikitokea hivyo basi nafikiri hii ajira itakuwa nzuri kuliko zote.
 
mtaweweseka sana na matokeo ya kitihani ya taifa!nyie paruaaneni weeeeee lakini msidharau kazi za wenzenu!
mimi ni mwalimu
KIDATO CHA NNE NINA DIVISION 2
KIDATO CHA SITA NINA DIVISION 1.9
DEGREE NINA G.P.A YA 3.7
kwa taarifa yako yapo mengi sana yanapaswa kubadilishwa lakini mkibaki na imani kuwa walimu ndio chanzo tutazidi kuumia sana kama taifa! na serikali yenu ndo upopo inaowajaza huo kichwani!
nyie endeleeeni tu!

kwa kuwa wote tunasapoti mwl ana alama za chini za ufaulu, basi wote hata kama una dv 1 ni vilaza zaidi ya walimu. Tumefundishwa na waliofeli hao hao wakatutungia mitihani wakasahisha wao na makis wakapanga wao mwisho wakatupa matokeo mabov zaid ya waliyoyapata halafu leo tunakumbuka LAKINI HAWA SI WALIFELI. Watanzania tuache kuchana mbeleko iliyotubeba.
 
................niliweza kujiendeleza na mpaka sasa ni mwl lkn nafanya kazi kama environment toxicologist and lab scientist.

sipendi jinsi ambavyo watu huona kaa fani ya ualimu ni ya watu waliokosa pa kwenda, kwani sio kweli wengi huwa tunaingia tukiwa na tegemeo la ajira mkononi ila huko kwenye ajira yenyewe ndiko kunako katisha tamaa na kutufanya wengi wetu kuchepuka kwenye fani nyingine.......

Umeona eeehhh, sasa tunaongea lugha moja, haiwezekani mtu yuko vizuri akaingia huko kwa kupenda ni namna tu ya kupita kama ulivyoeleza. Sasa watu wa aina kama yako wakibaki kufundisha ndo tutapata mabadiliko chanya katika elimu yetu. Na nafikiri sasa nakuona umenielewa kwamba hata kama watu kama wewe mkisoma ualimu kama hamjaenda kufundisha, tatizo litakua palepale kwa sababu watakao baki kufundisha ni wale wasio kama wewe, watafundisha wale niliowataja kwenye post zangu huko nyuma.

Naona unaonekana ulisoma PCB, mimi ni jirani yako nilisoma PCM miaka ya nyuma kidogo na hapo UDSM nilitoka 1998, kwa hiyo hayo ya miaka ya nyuma nayafahamu vizuri pia. Nashukuru kunikaribisha ofisini kwako nitafika siku moja.
 
sio kweli kwamba waalimu walioko mashuleni ni vishoka na kwamba wajanja wamesepa hapana. wengine wapo na ana nia nzuri tu ila kwann wanafunzi wanafeli waje watuulize tutwajibu ukweli wote.
 
Mwanang fanya reseach kwanza ndo u display coz c kwel kwamba waliopata division one na two hawajaenda ualim mfn uds udm na viuo vingine wapo weng
 
wachawi ni makonda madereva wa daladala na waendesha bodaboda, makonda na madereva wanawaacha wanafunzi hivyo muda mwingi anawaza usafiri badala ya kuwaza biology, bodaboda wanawapeleka gest wakapigwe maji n a wanawapakiza kwa makubaliano ya baadae kuwageda
 
Ni kweli lakini in %wise hizo sababu zako zitakuwa na 0.0001%, na hicho ndicho selikali inajaribu kuwapotosha raia kuwa watoto siku hizi hawana nidham, ooh! watoto wameharibiwa na facebook kitu ambacho mimi naona nikupotosha umma maana tunazungumzia sababu ambazo zote ukizijumulisha hazifikii 10%, kuanzia saa2 asubuhi mpaka saa8 mchana hata mwalimu mmoja hajaingia dalasani unadhani kwa umri wa wanafunzi watafanya nini kama sio kupiga stori za wachumba na facbook, siminari hiki kitu hakipo kwa sababu mwalimu anatoka darasani mwingine kusubili mlangoni na kila mwalimu anaacha zoezi kesho atakagua mda wa kupiga stori za facbook zitapigwa saa ngapi, zaidi ya 78% ya wanainchi wa tz wanatoka vijijini hawa hawana uwezo wa kumiliki simu, naamini zaidi ya 80%ya wanafunzi hawana simu cha msingi selikali iwakumbuke na kuwaheshimu walimu kama enzi za mwalim au inchi nyingine haya matatizo naamini yatapungua sana na hili litakua gumu kama familia za viongozi hawatasoma shule za selikali
 
Funika kikombe mwana haramu apite ama ni upepo tu utapita ndicho ambacho viongozi wetu wanakifanya kwa fikra zao za kutokuona mbali
 
Huwezi amini pamoja na wanafunzi kuvunja record ya kuferi eti kiwango cha kupasi kimepandishwa, sasa mwakani sindo wataferi malambili ya huu uliopita
 
Back
Top Bottom