Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Azarel kaandika maneno hayo hapo chini:
"Nyerere alikuwa mwerevu na mwenye uwezo mkubwa wa kuongoza.
Aliwafumbua macho wacheza bao, wale wavaa kobasi waliokuwa na Ilmu Akhera tu." Azarel (JForum)
(Nimesahihisha makosa ya ucharazi na wapi iwe herufi kubwa au ndogo) ila nimeacha ''kobasi,'' iwe hivyo kwa sababu maalum.
Kauli hii imenitia hamu nipitie picha zilizoko ndani ya kitabu cha Wasifu wa Julius Nyerere na kwa bahati mbaya sikukuta picha za watu hawa, ''wacheza bao, wavaa kobasi walikuwa na Ilmu Akhera tu,'' chembelecho Azarel.
Lakini mimi ninazo picha za hawa wacheza bao nk. pamoja na wavaa mabaibui katika Maktaba yangu ambayo waandishi wa Wasifu wa kitabu cha Julius Nyerere wamesema ni kati ya maktaba tatu bora - maktaba ya Salim Ahmed Salim, Hashim Mbita na ya Mohamed Said.
Picha ya mbali kabisa wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika katika maktaba yoyote ni hii ya Wazee wa TANU walipigana Nyerere.
Picha hii ilipigwa mwezi August 1954 baada ya Kamati ya UNO kuzuru Tanganyika kuja kusikiliza maoni ya wanannchi.
Said Chamwenyewe ndiye aliyewakilisha maoni ya Watanganyika akiwa mjumbe katika Baraza la Wazee wa TANU Dar es Salaam, Makao Makuu, New Street.
Said Chamwenyewe ndiye aliyeiletea TANU wanachama wake wa kwanza kutoka Rufiji.
Baraza la Wazee wa TANU ndiyo waliyotayarisha safari ya Territorial President wa TANU Julius Nyerere kwenda UNO February, 1955
Picha nyingine ya zamani sana ni ya Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU akiwa na Julius Nyerere na John Rupia kwenye tawi la TANU alilofungua Ali Msham nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa 1954/55.
Hao nyuma ya viongozi hao wa TANU ni Bantu Group kivazi chao ni hizo kaniki na wamebeba silaha za jadi mashoka, mikuki na pinde kwa ajili ya ulinzi wa viongozi wapigania uhuru wa Tanganyika.
Picha nyingine ni ya akina mama wavaa mabaibui wakimsindikiza Julius Nyerere Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam safari ya kwanza UNO 1955.
Picha ya mwisho ni ya wazalendo Iddi Faizi Mafungo Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) na Mweka Hazina wa TANU kavaa kobazi, kanzu na tarbushi na Sheikh Mohamed Ramia kavaa kobazi, kanzu na kofia wakiwa na Julius Nyerere wakitembea majimboni kuwahamisisha wananchi kujiunga na TANU kudai uhuru wa Tanganyika.
Picha hiyo imepigwa Dodoma Railway Station mwaka wa 1955.
Picha hizi zinatosha kuwa jibu kwa Azarel kuwa Nyerere hakufika Dar es Salaam akapokewa na watu wajinga kama anavyodhani.
Picha haisemi uongo.
Camera inaona kile jicho kilichoona.
Picha pia inasema maneno elfu moja.
Leo hawa wazee wangu waliompokea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa mapenzi makubwa anatoka mtu anawatusi kwa sababu tu hawakuwa wavaa suti walikuwa wavaa kobazi kanzu na wakicheza bao.
Labda katika kitabu cha Wasifu wa Julius Nyerere wazalendo hawa wangelitajwa na picha hizi zikawepo wazee hawa wangepata heshima ile ile anayopewa Mwalimu Nyerere kama mpigania uhuru.
Haya yanatosha ingawa yapo mengi na picha nyingi za kuweka.